Waislamu wahimizwa kuchangia maendeleo

MaxShimba

JF-Expert Member
Apr 11, 2008
35,772
4,054
WAISLAMU nchini wametakiwa kujitokeza na kuunga mkono uchangiaji wa shughuli mbalimbali za maendeleo hususan elimu, ili kujikwamua na lindi la umaskini. Wito huo ulitolewa juzi na Mbunge wa Temeke, Abbas Mtemvu, na mdhamini wa CCM Kata ya Mbagala, Aisha Sururu, katika harambee ya uchangiaji wa Kituo cha Asw-habulkahfi Islamic iliyofanyika huko Yombo Davis Corner jijini Dar es Salaam.

Harambee hiyo iliandaliwa baada ya madrasa hiyo ambayo hivi sasa inafanya shughuli zake Kariakoo kununua kiwanja kwa ajili ya ujenzi huko Yombo ambako kwa jana zilichangwa sh 375,000.

Akizungumza baada ya harambee hiyo, Mtemvu aliwasihi Waislam wengine kuzidi kukichangia Asw-habulkahfi Islamic Centre, kwani kitawawezesha kuwa karibu zaidi na hivyo kusaidia katika jukumu la kuiletea maendeleo jamii. Mtemvu pia katika harambee hiyo, aliwahakikishia wananchi wa Jimbo la Temeke kuwa ahadi yake ya ujenzi wa barabara si kiini macho, kwani ameishaanza kuitekeleza kwa vitendo tofauti na baadhi ya watu walivyoanza kupotosha ukweli.

"Ndugu zangu Wanatemeke nawahakikishia ahadi yangu ni ya kweli na utendaji umeishaanza na bado; tunaendelea kuboresha na kujenga barabara, hivyo nawaomba muwe na subira wakati huu wa utekelezaji," alisema Mtemvu. Mbunge huyo alibainisha kuwa, tayari zimepatikana sh bilioni 3 na utaratibu wa kuwapata makandarasi unaendelea kwa ajili ya ujenzi wa barabara kutoka Jet hadi Tandika.

Kwa upande wake, Aisha Sururu, katika kusaidia ujenzi huo ufanikiwe, ameanzisha vikundi vya uchumi kwa kinamama, ili wajiwezeshe kiuchumi hivyo kujiletea maendeleo.

Alisema Uislam unazidi kudidimia kutokana na Waislamu kujitenga na kukosa elimu, hivyo aliwataka kinamama kubadilika na kuungana na vijana wao katika kujiletea maendeleo.Chanzo: Gazeti la Tanzania Daima
 
Back
Top Bottom