Mkulima na Mfugaji
JF-Expert Member
- Jul 26, 2013
- 1,057
- 1,868
Sifa njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (SwallaAllaahu 'alayhi wa aalihi wasallam) na Swahaba zake(Radhiya Allaahu 'anhum) nawatangu wema mpaka Siku ya Mwisho.
Naona kuna mijadala mingi imezuka kuhusu Albadir Awali Nataka kurekebisha ibara hiyo kwani sivyo inavyokusudiwa au inavyotamkwa au kuandikwa. Ibara hiyo imetoka katika lugha ya Kiarabu lakini kupotolewa au kuandikwa na kusomwa makosa katika Kiswahili.
Wapo wanaosema Alibadiri lakini makusudio ni Ahlul-Badr, yenye maana watu wa Badr(wale waliopigana vita vya Badr). Badr ni sehemu iliyokaribu na Madiynah na ndio iliyokuwa sehemu ambayo Waislamu wakiongozwa na Mtume (Swalla Allaahu 'alayhiwa aalihi wa sallam) walipambana na mushirikina wa Makkah katika vita vya kwanza baina ya pande hizo mbili.
Waislamu waliohudhuria walikuwa baina ya 313 – 317, lakini pamoja na idadi yao ndogo hiyo waliweza kuwashinda washirikina waliokuwa na idadi kubwa ipatayo mara sita yao. Kisomo cha Ahlul Badrii na kuwa ni kutaja majina ya Maswahaba (Radhiya Allaahu‘anhum) mmoja baada yamwingine.
Katika kutaja huko ni Imani ya mwenye kusoma hao Maswahaba (RadhiyaAllaahu ‘anhum) wanamsaidia kwa njia moja au nyingine. Ima kupata kitu alichopoteza au kilichoibiwa au kulaaniwa aliyefanya.
Na hii katika Uislamu ni njia moja ya shirki ambayo Allaah Aliyetukuka na Mtume Wake (Swalla Allaahu'alayhi wa aalihi wa sallam)wameikema na kuipiga vita sana. Allaah Aliyetukuka Anasema:“ Hakika Allaah Hasamehe kushirikishwa, na husamehe yaliyo duni ya hilo kwa Amtakaye. Na anaye mshirikisha Allaah basi hakika amezua dhambi kubwa” (4: 48). Shirki ni dhuluma kubwa sana.