Leo napenda ku share hii na wana jamvi wenzangu kuhusu tatizo la kukosa ajira,
Wahitimu wenzetu wa nchi ya Rwanda baada ya kuona ukubwa wa tatizo la ajira,
Wao wenyewe hivi sasa wakimaliza chuo tu, badala ya kuanza kupambana na kutafuta ajira kisha kukutana na bango kubwa HAKUNA KAZI, Sasa baada ya kuhitimu shahada ya kwanza wanaenda vyuo vya ufundi stadi kujifunza fani mbalimbali kama upishi,kuchomelea,useremala, mitindo(design),umakenika,Kilimo,Ufugaji, ujenzi na mengineyo, Lengo ni kwamba ukiwa na ujuzi wa moja kwa moja angalau utaweza kujiajiri pasipo kutegemea mtaji kwa kiasi kikubwa na ujuzi wako kuwa mtaji wako na hivyo kuweza kusonga mbele pasipo kusubiria ajira za maofisini
KWETU SISI WAHITIMU WA KITANZANIA. Ni vema na sisi tukaiga mfano huo wa majirani zetu, kwani sasa hali katika soko la ajira sio nzuri na miaka inavyozidi kwenda ndio hali inazidi kua taabani na hakuna matumaini hata kidogo kutokana na wahitimu ni wengi katika soko kuliko nafasi mpya za ajira zinazozalishwa kila mwaka.
Kuliko kuendelea kulalamika siku hadi siku ni vema tukachukua hatua ya kutatua tatizo hili kwa namna nyingine.
TAFAKARI,CHUKUA HATUA
Ahsante