Makaayamawe
JF-Expert Member
- Feb 21, 2009
- 341
- 10
Wahindi wawili wafia hotelini Dar
Na Mwanaidi Swedi
8th June 2009
Wahindi wawili ambao mmoja ni raia wa Canada na mwingine wa Afrika Kusini wamekutwa wamefariki dunia katika mazingira ya kutatanisha ndani ya vyumba vya hoteli ya Harbours View iliyopo kwenye jengo la JM Mall Jijini.
Kamanda wa Polisi katika Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Seleiman Kova, ameiambia Alasiri leo asubuhi kuwa miili ya wahindi hao ilikutwa katika vyumba tofauti vya hoteli hiyo, majira ya saa 8:00.
Akielezea zaidi, Kamanda Kova amesema kuwa Polisi walipata taarifa toka kwa Meneja Masoko wa hoteli hiyo aitwaye Bw. Laizer Manukwa, aliyeeleza kuwa usiku, kuna mteja wao aliyekuwa chumba namba 10-12, aliyefahamika kwa jina la Sulman Zuber, 41, Mhindi aliye raia wa Canada, alikutwa akiwa amekufa chumbani humo.
Kamanda akasema kuwa katikaå tukio jingine lililojiri hotelini hapo, ilibainika kuwa katika chumba 12- 09, ghorofa ya pili, mtu aitwaye Nickel Kumar Taluar, 33, raia wa India, alieleza kuwa mpangaji mwenzie ambaye pia ni mhindi aitwaye Yusuf Seda, raia wa Afrika Kusini, alikutwa pia amefia chumbani kwake.
Aidha, Kamanda Kova akasema kuwa vifo vya watu hao wanaodaiwa kuwepo hotelini tangu Mei 19 mwaka huu havionyeshi kuwepo na purukushani yoyote kabla ya kutokea kwake.
Hata hivyo, akasema taarifa za awali toka kwa uongozi wa hoteli hiyo zinaonyesha kuwa watu hao walirejea jana alfajiri toka kwenye sehemu za starehe na kwamba kuna wakati, mwingine alionekana kwenye maeneo ya Casino ya hotelini hapo.
Akasema inawezekana walikuwa wamezidisha vinywaji walipokuwa katika maeneo hayo.
Akasema kutokana na tukio hilo, Polisi wameunda timu ya wataalam mbalimbali akiwemo Mkemia Mkuu na Daktari ili kuweza kubaini chanzo cha vifo vya watu hao.
Akasema upelelezi unaendelea na hadi sasa hakuna aliyekamatwa kuhusiana na tukio hilo.
Akasema inawezekana walikuwa wamezidisha vinywaji walipokuwa katika maeneo hayo.
Sio tu ni mbaguzi bali pia mnyanyapaaji. lugha ya Kitanzania sio hiyo. Zeruzeru tunawaita walemavu wa ngozi; bubu walemavu wa ulimi; viziwi tunawaita wasiosikia; hani*** tunamwita sio rizki.....Mhhh.. sasa huyu aliye andika hii habari naye tumuite mbaguzi? kwa vile kasema wahindi wawili.. pengine angesema watu wawili wenye asili ya Asia.. (sorry wakuu naona ndivyo wabongo tunavotakiwaga tuseme hasa tunapo zungumzia wageni nchini kwetu!)
Mhhh.. sasa huyu aliye andika hii habari naye tumuite mbaguzi? kwa vile kasema wahindi wawili.. pengine angesema watu wawili wenye asili ya Asia.. (sorry wakuu naona ndivyo wabongo tunavotakiwaga tuseme hasa tunapo zungumzia wageni nchini kwetu!)
......sisi waenda kwa miguu/wapanda dalaX2 twawaita wenye mashangingi mafisadi,wafanya biashara wazalendo twawaita fisadi papa,wasio wazalendo twawaita fisadi nyangumi....Sio tu ni mbaguzi bali pia mnyanyapaaji. lugha ya Kitanzania sio hiyo. Zeruzeru tunawaita walemavu wa ngozi; bubu walemavu wa ulimi; viziwi tunawaita wasiosikia; hani*** tunamwita sio rizki.....
Sio tu ni mbaguzi bali pia mnyanyapaaji. lugha ya Kitanzania sio hiyo. Zeruzeru tunawaita walemavu wa ngozi; bubu walemavu wa ulimi; viziwi tunawaita wasiosikia; hani*** tunamwita sio rizki.....
I like the way you have written your comments.imenichekesha sana. Inawezekana tuna kawaida ya kutumia njia ndefu kwenye safari ambayo inawekekana kwa njia fupi. Maana nimefikiria kuwa, hata mtu akiiba, tena akiwa kigogo, ukimwita mwizi unaweza ukaambiwa umekosa heshima mana wezi wako uswazi tu.Wao hawaibi...wanafanyaje sijui??!!Sio tu ni mbaguzi bali pia mnyanyapaaji. lugha ya Kitanzania sio hiyo. Zeruzeru tunawaita walemavu wa ngozi; bubu walemavu wa ulimi; viziwi tunawaita wasiosikia; hani*** tunamwita sio rizki.....
Hii ndo nchi pekee unakuja maskini halafu unaiba big time na kuwa milionea kama umesimama. Siwachukii hawa jamaa ila imefika sehemu tuanze kuwa makini na wanayoyafanya.Wanaiharibu TZ na siku ya kugundua hilo hatutakuwa na wakulia nao maana watakuwa wameenda Canada na UK.Wengi hawana nia nzuri na TZ. period!Rwabugiri,
Lugha iliyotumiwa ni sahihi kabisa.
Watu wawili wenye asili ya Asia sio sahihi na pia sio lazima wawe wahindi. Wanaweza kuwa yeyote tokea Palestine mpaka Japan.
Lisilo la kawaida ni kwa Wahindi kufurika nchini na kufia huko kiajabu ajabu.
Yaani wote wawili wazidiwe na kilaji kiasi cha kupoteza maisha......!
Kusema wahindi wawili na watu wawili wenye asilia ya Asia whats the difference?Mhhh.. sasa huyu aliye andika hii habari naye tumuite mbaguzi? kwa vile kasema wahindi wawili.. pengine angesema watu wawili wenye asili ya Asia.. (sorry wakuu naona ndivyo wabongo tunavotakiwaga tuseme hasa tunapo zungumzia wageni nchini kwetu!)
Mbona sioni R.I.P. Wahindi?
kwikwikwikwikwikwi watz wanafiki......Mbona sioni R.I.P. Wahindi?
Kusema wahindi wawili na watu wawili wenye asilia ya Asia whats the difference?