Wahi maeneo boko

Ellie

Senior Member
Sep 2, 2011
123
15
Boko dsm kuna viwanja vinauzwa kimoja 20m kwa 20m,viko hatua chache kutoka barabarani almost mita 300.
 
Nina hela ya kununua kiwanja lakini sina hela ya kukupigia simu,kama umeamua kutangaza kuwa unauza kiwanja weka na bei yake,kila mtu ajipime,sio namaliza salio langu kuuliza bei wakati bei yenyewe iko tofauti na kiwango nilichofikiria ,hatimaye hakuna wakunilipa salio langu nililopoteza kupiga kuulizia kiwanja,
 
Sijui ni watanzania au ni baadhi ya watu tuna/wana matatizo sana, wewe kama ni muungwana na umeamua kuweka tangazo online kuwa unauza kitu au unataarifa ya kitu fulani kuuzwa , kwa nini usiendeleleze uungwana wako kwa ku-exhaust details zote muhimu, mfano kama ni kiwanja eg mbezi juu, mita 40*40, bei makisio Mil 9 , umbali toka barabarani KM ...., namba ya muhusika ni 07.....,

Vile vile n agari, laptop, simu nk. yani mtu anakurupuka kuwa nauza gari , zuri sana anayetaka anipm sasa kuna maana gani ya kutumia forum ambapo wote wanaona. Tusaidiane na kupunguza urefu wa thread, kama una information weka zote kama huna sema nina fununu kuna simu inauzwa ila sina uhakika wa bei basi utapunguza maswali.
 
Back
Top Bottom