Wahandisi; NISAIDIENI KATIKA HILI | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wahandisi; NISAIDIENI KATIKA HILI

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Amoeba, Jan 4, 2012.

 1. Amoeba

  Amoeba JF-Expert Member

  #1
  Jan 4, 2012
  Joined: Aug 20, 2009
  Messages: 3,328
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 0
  Nina kiwanja changu milimani nataka kujenga, tatizo ni kwamba pamoja na kuwa eneo limepimwa na barabara zipo katika ramani, barabara hizo hazijachongwa na hakuna mpango wa manispaa kufanya hivo hivi karibuni. Swali langu ni kuwa,
  1. je inawezekana mimi binafsi nikajitolea kujenga barabara inayoelekea kwangu kwa kiwango cha changarawe (Mita 300) na kama ndiyo, natakiwa nifuate taratibu zipi kupata kibali cha kufanya hivyo? na je, umbali huo unaweza kunigharimu kiasi gani cha pesa?
  2. Kutoka mwanzo wa shamba langu mpaka ninapojenga ni umbali wa mita 200, je itagharimu kiasi gani kujenga barabara ya (a) changarawe (b) Lami (c) zege pavements? Ipi ni nzuri kwa sehem hiyo?
  Eneo lenyewe ni ardhi ngumu yenye mawe na changarawe nyingi.
  Naomba pia bei ya kukodi grader (gari la kusawazisha uwanja) kwa saa, na conditions zake!
  IRINGA.


  ANGALIZO: SIJATANGAZA TENDA NA SINA MPANGO HUO! Kwa hiyo PM ni za free consultancy tu!
   
 2. M

  MWENDAKULIMA JF-Expert Member

  #2
  Jan 4, 2012
  Joined: Jul 17, 2009
  Messages: 961
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 35
  Mkuu,
  1.Kwa swali lako la kwanza ningependa kujua unayotaka kujenga ni private au public road? i'm a bit confused na huo umbali ulioutoa hapo juu na kwenye swali lako la pili. Kama ni private kwa maana ya hata hiyo barabara unayotaka kuijenga ipo within your compound haina shida endelea tu na ujenzi kwa viwango unavyovitaka and no body will question.Ila kama ni part of the public road inabidi uende manispaa/mji elezea kusudio lako na watakupa specifications and/or terms zinazotakiwa kutimizwa kabla na wakati wa ujenzi

  2.Katika estimate ya ujenzi kuna factors nyingi zinazodetermine cost ya ujenzi kwa mfano kama unataka kujenga kwa changarawe je zinapatikana wapi?cost per trip ni ipi?na unataka kujenga ya standard gani?(kumwaga tu changarawe na kuacha ushindiliaji ufanywe na traffic/magari wakati ikiendelea kutumika au kushindilia kifusi kwa roller baada ya kusambaza kwa mkono/grader).The most cost-efficient way ni kutumia grader/bull dozer wakati wa clearance/usafishaji wa mwanzo kama hiyo ni barabara mpya kabisa,utatumia lorries/tippers kuleta kifusi na kukimwaga kulingana na unene wa kifusi unachokitaka baada ya kusambaza thereafter utatumia manual labor kusambaza then utalazimika kukodi water bowser na roller kwa siku moja kumalizia umwagiliaji maji na ushindiliaji.Sikushauri kujaribu aina hizo nyingine za barabara kwa urefu wa barabara yako na nature of the soil(kama ipo kama ulivyoelezea),it's simply uneconomical lakini kama umedhamiria you can PM me for they(asphalt,surface dressing,rigid/concrete pavements) are a bit more complex.

  Kuhusu gharama za kukodi grader kwa sasa sijui upo mkoa gani maana zinavary from place to place ila hakikisha una kiasi kisichopungua 1.2m majority hukodisha kwa siku ( masaa 8 huhesabiwa ni siku moja na normally ni dry lease mafuta juu yako).


  Nimejitahidi kukujibu kwa ufahamu wangu inaweza kuwa sijajibu kila kitu but something is better than nothing,isn't it? unaweza kuuliza maswali mengine kama unayo
   
 3. N

  Ngereja JF-Expert Member

  #3
  Jan 4, 2012
  Joined: Feb 27, 2007
  Messages: 796
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 45
  Kwa nini unataka kusawazisha kiwanja? unaweza save hizo gharaama kwa kujenga pasipo kusawazisha, labda kama ni lazima na hakuna jinsi. Unachotakiwa kufanya ni kuchora ramani ya topografia ya kiwanja chako, kisha mpe msanifu majengo akusanifie ramani "according to topography, then mwisho wa ujenzi fanya landscaping. Utakuwa umemaintain stability ya udongo kwenye kiwanja.
   
 4. Amoeba

  Amoeba JF-Expert Member

  #4
  Jan 5, 2012
  Joined: Aug 20, 2009
  Messages: 3,328
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 0
  Wasalaam,
  Heshima mbele kama ilivyo ada kwa Waungwana! Nashukuru sana mkuu kwa kunijibu kwa ufasaha na kunipa mwanga wa wapi pa kkuanzia, kwa ufafanuzi zaidi tu ni kuwa.

  1. Kama nilivyobainisha hapo juu, umbali wa Mita 300 ni public road, na umbali wa mita 200 ni private, kwa maana jumla ya hapo ni mita500.
  2. Site iko iringa mkuu, na lengo ni kuwa na barabara nzuri, kwa maana kumwaga kifusi na kushindilia! Kwa hiyo Mkuu hapo kwenye Grader, kama 8hrs ndy siku moja ina maana masaa 24 ni siku tatu ambzo zitacost 3.6M bila mafuta? Vipi kuhusu makadirio ya mafuta (najua inategemea na aina ya mashine) lakn nataka kupata tu makisio ya hesabu ya kuanzoa. Vipi kuhusu operator wa hiyo mashine, analipwa na mmiliki au namlipa mm, kama namlipa mimi ni wastani wa bei gani?
  Heshima kwako Mkuu.
   
 5. Jaguar

  Jaguar JF-Expert Member

  #5
  Jan 5, 2012
  Joined: Mar 6, 2011
  Messages: 3,409
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Mh!mimi ni land surveyor hapa hapa Iringa kampuni ya Interbeton lakini siwezi kukupa makisio unayoyataka,ngoja niongee na mwenzangu upande wa quantity survey.
   
 6. M

  MWENDAKULIMA JF-Expert Member

  #6
  Jan 5, 2012
  Joined: Jul 17, 2009
  Messages: 961
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 35
  Nashukuru mkuu kwa maelezo ya ziada

  1. Kwa hiyo for those 300m itakubidi uende manispaa kama nilivyobainisha hapo juu,nadhani kwenye hili hakuna tatizo.
  2.Kwa kawaida ukienda kwa kampuni/mtu who leases out those sort of equipments kuna makubaliano yanafanyika.Nilikupa dondoo kidogo ya nature ya contracts nyingi za ukodishaji wa grader nilipozungumzia hiyo 8hrs.Upo sahihi siku ina 24hrs,lakini kwa kazi za barabara hatutegemei ufanye kazi beyond 1800hrs(saa kumi na mbili jioni) kwa hiyo say grader inaanza kazi saa mbili asubuhi kama kuna 2hrs za lunch break ina maana ikifika saa kumi na mbili jioni hayo yatakuwa ni masaa 8 (siku moja imeisha) unapark grader.Kwa kawaida kama sehemu ya barabara inayokuwa graded haijaharibika sana yaani haimchukui operator muda mrefu kupata muonekano unaotakiwa wa barabara(road prism) kwa hayo masaa manane ukiwa na operator mzoefu unaweza kufanya up to 1.2km.Nilikupa estimate ya 1.2m to be on the safe side,operators normally hulipwa at least 20,000/day(say wewe utamlipa 30,000).Diesel makadirio ni 20litres/hr (nakupa makadirio under the worst case scenario for consumption/hr differs kulingana na type ya machine na mechanical soundness).Na ili kuwa economical make sure clearing & grubbing (uondoaji wa visiki,miti na obstacles nyingine unafanywa mapema otherwise you will need to hire a bulldozer beforehand kama hivyo nilivyovitaja ni vingi na haviwezi kuondolewa kwa hand tools).Issue ya roller na water bowser siyo kubwa hizo ndizo mashine zinazokodiwa kwa bei nafuu zaidi kwenye kazi za ujenzi.

  Samahani mkuu kwa maelezo marefu,kama kuna kitu haujakielewa uliza.

  NB. Acces ya internet ni ya shida kidogo ndiyo maana nimechelewa kidogo kukujibu.
   
Loading...