wagonjwa washinda kwenye vyandarua mchana | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

wagonjwa washinda kwenye vyandarua mchana

Discussion in 'JF Doctor' started by MziziMkavu, Mar 11, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Mar 11, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,611
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  [​IMG]


  Na Jumbe Ismailly,Singida
  Kituo cha afya cha Sokoine,kilichopo katika Manispaa ya Singida kinakabiliwa na tatizo la kuwa na mbu wengi nyakati za mchana,hali ambayo hutishia wagonjwa wanaolazwa kulazimika kukaa ndani ya vyandarua hata nyakati za mchana kwa kuhofia kuumwa na hatimaye kuambukizwa ugonjwa wa malaria. Malalamiko hayo yalitolewa na wagonjwa waliolazwa kwenye kituo hicho,kwa Naibu Waziri wa afya na Ustawi wa jamii,Dk.Aisha Omari Kigoda aliyetembelea kituo hicho na kuzungumza na wafanyakazi pamoja na akina mama wajawazito.

  Aidha walisema akina mama hao kuwa ni jambo la kawaida kwenye kila nyumba au kituo cha afya kuwepo mbu nyakati za usiku,lakini kwenye kituo hicho ni kinyume kabisa kwani hulazimika kukaa ndani ya vyandarua hata nyakati za mchana.

  “Tumekuwa tukikaa ndani ya vyandarua hivi hata mchana kutokana na kuogopa kuumwa na wa na ambao wanaweza kuwaambukiza malaria

  mbu waliogeuza makazi yao kwenye wodi za kituo hiki cha afya kutokana na kutopigwa dawa za kuwauwa mbu hawa”alisikika mmoja wa wagonjwa waliolazwa akimweleza Naibu waziri  Hata hivyo walibainisha kwamba wamekuwa wakiulalamikia bila mafanikio uongozi wa kituo hicho kuhusu hofu yao ya kupona magonjwa yaliyowafanya walazwe na badala yake kuondoka na ugonjwa wa malaria.  Hivyo kutokana na hali hiyo ambayo kila mgonjwa aliyelazwa amekuwa akiongea na watu waliokwenda kumsalimia huku akiwa ndani ya chandarua ,wamemuomba waziri mwenye dhamana kuangalia uwezekano wa kukipatia kituo hicho dawa za kutosha za kupulizia kwa ajili ya kuua mbu hao ili waweze kuepukane na ugonjwa huo.  Akiongea na watumishi wa kituo hicho,Naibu Waziri wa afya na Ustawi wa jamii,Dk.Aisha Omari Kigoda alisema kwamba madhumuni ya ziara hiyo ni kufuatilia yale yote yaliyoahidiwa kutekelezwa kwenye ilani ya uchaguzi ya mwaka 2005.  Hata hivyo Naibu waziri huyo aliweka wazi kwamba ni ukweli usiopingika kuwa huduma zitolewazo kwenye kituo hicho hazitoshelezi kabisa mahitaji ya wateja wanaokwenda kupatiwa huduma.  Aidha Dk.Kigoda hata hivyo aliduwazwa na kundi la mbu waliokuwepo kwenye wodi alizotembelea,hususani ya akina mama wajawazito ambao kila mgonjwa aliyetembelewa alikutwa akiwa yupo ndani ya chandarua wakati alipokuwa akiongea na naibu waziri huyo.

   
Loading...