Wagombea wa CCM, endeleeni kuutafuta Ubunge lakini Uraisi mpeni Dr. Slaa

Mag3

Platinum Member
May 31, 2008
13,064
22,757
Kwa wagombea Ubunge kupitia CCM;

  • Kama kweli unakerwa na usanii wa serikali ya CCM chini ya Raisi Kikwete.
  • Kama kweli unachukia vitendo vya rushwa ndani ya serikali ya CCM.
  • Kama kweli unakerwa na uhuni wa viongozi wa CCM na serikali yake.
  • Kama umechoka na utawala mbovu usiojali haki wala kufuata sheria.
  • Kama unakerwa na EPA, Kagoda, Dowans, Richmond, Radar, Kiwira n.k.
Basi, pamoja na kuwaomba wananchi wakuchague uwe Mbunge wao, usisite kuwaomba wamachague Dr. Slaa wampe kura awe Raisi wao na kwa pamoja tushirikiane kulijenga taifa.

Na kwa wapiga kura wote;

  • Kama unalipenda Taifa lako na ungependa kuliona linaendelea
  • Kama ungependa kuona mabadiliko ya msingi pamoja na katiba.
  • Kama unataka kuona heshima ya Tanzania kama taifa inarudi.
  • Kama ungependa kuongozwa na serikali inayowajali wananchi wake.
  • Kama ungependa kuona sheria ikichukua mkondo wake dhidi ya dhulma.

Siku ya kupiga kura tujitokeze kwa wingi tulikomboe taifa letu kutoka mikononi mwa mafisadi kwa kumpigia kura Dr. W. P. Slaa. Nafasi kama hii hupatikana mara moja katika miaka mitano.
 
HTML:
Siku ya kupiga kura tujitokeze kwa wingi tulikomboe taifa letu kutoka mikononi mwa mafisadi kwa kumpigia kura Dr. W. P. Slaa. Nafasi kama hii hupatikana mara moja katika miaka mitano
asante kwa ujumbe murua.
 
Umeona watu waliojitokeza jangwani leo? slaa atawapata hao? kidogo Prof. Lipumba atawakaribia lakini kuwafikia itakuwa ngumu. You will see.
 
Umeona watu waliojitokeza jangwani leo? slaa atawapata hao? kidogo Prof. Lipumba atawakaribia lakini kuwafikia itakuwa ngumu. You will see.

Na wameshudia kwa mara nyingine Rais mtarajiwa akiangua! Walikuwa wana hamu ya kuona kama ataanguka ama la!
 
Back
Top Bottom