Mkalukungone Mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 2,437
- 5,235
Malalamiko yameibuka kutoka kwa baadhi ya Wagombea wa Ubunge kupitia kundi la Wanawake (Viti Maalum) Mkoani Kilimanjaro, wakimtuhumu Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) wa mkoa huo,Elizabeth Minde, kwa kukiuka taratibu za uchaguzi kwa kupeleka majina ya wagombea kutoka Moshi Mjini pekee na kuwaengua wagombea kutoka Wilaya nyingine.
Wagombea hao, waliokuwa wakisaka nafasi kupitia UWT, wamedai kuwa mchakato mzima wa uteuzi ulikuwa na upendeleo, ambapo baadhi ya viongozi wa UWT walikuwa tayari na "majina mfukoni" kabla hata ya uchaguzi kufanyika, hali iliyoathiri haki na uwazi wa mchakato huo na kutoa onyo la kurejesha kadi.
“Tulishiriki mchakato huu kwa imani, lakini majina yetu yakakatwa bila sababu za msingi, iwapo Kamati Kuu ya CCM haitarudia uchaguzi huu kwa haki, tuko tayari kurejesha kadi zetu za uanachama wa UWT,” walisema wagombea hao kwa nyakati tofauti ambao hawakutaka kutajwa majina yao.
Kupata taarifa na matukio yanayojiri kuelekea uchaguzi mkuu kwa kila mkoa ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025
Katika kile kinachoonekana kuzidisha sintofahamu hiyo, Mwenyekiti wa UWT Mkoa, Bi. Elizabeth Minde, anadaiwa kumsaidia mgombea Zuena Bushiri, ambaye ni mmoja wa waliopitishwa, na baadaye Mwenyekiti huyo wa UWT mkoa, kuonekana akihudhuria sherehe ya pongezi nyumbani kwa Zuwena, hali iliyozua maswali kuhusu uhalali wa nafasi hiyo.
Kwa upande wake Bi. Minde amekanusha vikali tuhuma hizo, akisema uchaguzi ulifanyika kwa haki na kwa kufuata taratibu za chama.
“Kusherehekea ushindi ni jambo la kawaida, mimi nisingeenda kula na watu wakati tayari nimeshapata ubunge, Mbunge aliyebaki Moshi ni Zuwena, na mwingine tuliambiwa ameenda Arusha, tungeenda kumfuata huko?” alihoji Minde kwa mshangao.
Hata hivyo, Bi. Minde amejibu kwa kusema kuwa kila nafasi moja ilipaswa kuwa na wagombea watatu, na kati ya watu 28 waliokuwa wamejitokeza, walihitaji tu majina sita kwa hatua ya mkoa, alisisitiza kuwa hakuna wilaya iliyoachwa kabisa.
“Tulichunguza ushiriki wa wagombea kwenye shughuli za chama, mchango wao na namna walivyokisaidia chama, hatukuangalia majina kwa misingi ya ‘anatoka wapi’ bali kwa vigezo vya uadilifu na mchango halisi,” Alisema Minde.