Wagombea Ubunge 2020

Wagombea Ubunge 2020

DISPLEI

Member
Joined
Oct 17, 2012
Posts
73
Reaction score
48
Nimekutana na watu kadhaa wanaoutaka Ubunge kwa mwaka 2020. Watu hao wako umri wa miaka ya 30 hadi 50. Wana elimu zao za juu lakini unakuta mtu kapigika kweli kweli na ana zaidi ya miaka 10 mtaani.

Wengine ni wa kiume hata kupanga chumba hawajaweza wanakula na kuishi kwa wake zao.

Wapo hata wadada umri huo huo wako kwa wazazi na walezi wao. Hata wazo la kuanzisha banda la chips hawajakuwa nalo, sasa Ubunge kweli ni mwepesi kiasi hicho?

kwa Ubunge ambao unahitaji maono makubwa katika karne hii watauweza au ndo kutafuta kushibisha natumbo yao na kutafuta nitoke vipi.

Karne hii na mwelekeo wa nchi tunahitaji wabeba maono na wenye uwezo wa kuthubutu kuanzisha wazo na kulisimamia. Wafanya mahamuzi kuhusu wagombea walitazame hili tupate wagombea sahihi sio wasaka tonge.
 
ipo haja ya kupunguza maslahi ya kibunge

Maslahi nadhani yanaangaliwa kwa mapana yakizingatia unyeti wa Ubunge pia kulinganisha na nchi zingine hasa jirani.!. Suala ni wapiga kura wawe makini na kuhakikisha kwa uwingi huu wa watia nia basi watendee haki nchi hii kwa kupigia kura watu wenye kuonyesha watakuwa wa faida kwenye Ubunge.

Mungu Ibariki Tanzania.
 
ipo haja ya kupunguza maslahi ya kibunge
suer mwaka huu umevunja record yani watu wameacha tahaluma zao eti kwenda gombea ubunge,ila nafikili swala sio kuteuliwa swala nikutaka kuonekana ili apo labda mbele waweze pata teuzi but why hata kama unaelim na umeamua kufanya siasa usianzie kwenye ata udiwani ili wananchi wakuelewe?
 
Back
Top Bottom