Wagombea ndani ya CCM ni patashika

Wasirra aliwahi kuiba kura za ubunge huko nyuma na kupewa adhabu ya kutogombea kwa kipindi fulani. Kwa hivyo anazo chembechembe za wizi kama walivyo wanaukoo wote wa ukoo wa panya.
Pia juzi tumebaini anataka kubinafisisha nyumba ya bodi ya sukari. Amejipigia debe ili arejeshwe kuwa waziri wa Kilimo na chakaula ili aweze kukamilisha mchakato huo kwa urahisi. Tunamwangalia kwa karibu. Hiyo nyumba ataisikia kwenye ndoto. Ni nyumba ya umma. Huyu ni kama wanaukoo wenzake - ukoo wa panya.
 

ila kakaa bure kwene nyumba watu bila kulipa kodi ya pango
 
Makundi ya kugombea uraisi yaiuwa ccm
 

Wasira hafiki kokote Kwani Kambi yake Ni wasanii watupu Na wana njaa hakuna mfano wakipewa pesa wanakula wenyewe huku Wasira Mwenyewe ni Kikongwe kama Mwai kibaki na Mugabe wa Zimbabwe, na Membe anasubiliwa kufikishwa Mahakama ya kimataifa juu ya wizi wa Pesa za Gadafi na Kifo cha utata Cha baloz wa libya , akina Jauary , mwigulu , mwandosya hao ni wasindikizaji tu Fainal lazima itakuwa Pinda vs Lowasa.
 

Wakimweka Membe kisha wakamshindanisha na kivuli lazima kivuli kitaibuka kidedea , Wasira, January , Mwigulu , mwandosya ni wasindikizaji tu, Hata wakagawa Mapesa watu watasunda na kujikausha , Ni pinda au Lowasa wanaweza kuwasumbua Ukawa , wengine wasubiri mwaka 2020 huko.
 
Just imagine kama wassira sasa ndiye raisi wa nchi hii halafu yuko UN anahutubia??

Mimi mwenyewe najiuliza hapa siujui zile picha za kwenye mabango ya kampeini yake yatakavyokuwa kituko mitaani. Watoto watakuwa wakikimbia wakiyaona kwakweli.
 

kweli mkuu hii ni team wasira at work hata mm nimeona. Yan mtu akijenga hoja zake utaona tu anavyoenda hadi mwisho utagundua nia yake thabiti nini.
 
Mimi mwenyewe najiuliza hapa siujui zile picha za kwenye mabango ya kampeini yake yatakavyokuwa kituko mitaani. Watoto watakuwa wakikimbia wakiyaona kwakweli.

Hujafa hujaumbika....Usitukane wakunga na uzazi ungalipo!!Hakuna Mwandamu aliyejiumba...Tafakari kauli zako.Hata kama humpendi,usitumie maumbile yake kumdhuhaki
 
Wasira licha ya kuwa ccm, mi ninamkubali ni mwanasiasa asiye teteleka pia ni mwanasiasa anayeweza kujenga hoja na ndiye msafi kwani wale wanasiasa mafisadi huwa hawapendi kuonekana mbele ya macho ya kuoga kuumbuliwa wasira amekuwa mpiganaji nyuma ya wananchi hivyo namuombea mambo yake yaende sawa ili aingoze tanzania
 
Wotemagarasa hakuna mwenye unafuu kweli CCM ya sasa imeishiwa huyu Wasira mpanga njama za kuuwa watu wapinzani akishirikiana na Mwigulu atatawala wapi

Alipanga njama gani mkuu mbona mi huwa namwonaga ni MZEE ambae Hana shida
 

Pinda yupi huyu Huyu lege lege au yupi?
Pinda Huyu anaewategemea akina bulembo au yupi
Bora WASIRA au Lowassa lakini sio huyo mfuga nyuki
 

Unachembechembe za kike OVER
 
CCM haina mgombea anayefaa. Huu siyo uchaguzi kama wa 2005 ambapo mgombea alichaguliwa bila vigezo. Unafahamu kucheka na watu, unahudhuria misiba na kula nyama choma kwenye magenge na wananchi wa kawaida, tayari unafaa kuwa Rais.

Kwanza wananchi wote, hata tusiokuwa viongozi wa umma tunatakiwa kuwa waadilifu kwa maana ya kutokuwa na kashfa zinazokufanya uonekane ni mhalifu. Kutokuwa mwizi na kutokuwa na kashfa siyo sifa za kuwa Rais, hizo ni sifa za kuwa raia mwema.

Anayeutaka Urais, inabidi awaambie Watanzania amefanya nini cha pekee kila mahali alipokuwa tofauti na raia wengine wote, kiasi cha yeye kuona anafaa kuwa kiongozi mkuu, kuwazidi wengine wote. Kwangu mimi kwa hao uliowataja sijaona chochote:

1) January Makamba - Ni Naibu Waziri; amefanya nini cha pekee kwa nafasi aliyo nayo?

2) Bernard Membe - Business as usual; ana nini cha pekee?

3) Pinda - He is a below average performer, nafasi aliyo nayo ni kubwa mno ukilinganisha na uwezo wake

4) Nyalandu - Not worth for discussion; poor performer

5) Sumaye - Anaweza kubebwa na utendaji kazi wa Mkapa

6) Wasira - Hata jina lake likitajwa halileti ujumbe wowote wa kuelezea kitu anachosimamia

7) Lowasa - Sipendi Lowasa awe Rais but he was a leader. Jina lake likitajwa linaleta ujumbe/hisia katika moyo wako. Alisimamia sana masuala ya elimu, na pia ana ujasiri wa kutamka na kusimamia anachokiamini

Kiongozi mzuri anatoka nje ya CCM

1) Dr. Wilbroad Slaa - Likitajwa tu jina lake ujumbe unaoupata ni mtu jasiri, asiyeogopa chochote, mtu mwenye kujitofautisha kiutendaji kila mahali alipowahi kupewa nafasi. Alipokuwa kasisi wa Kanisa Katoliki, alionekana mapema na maaskofu kumwamini kuwa mtendaji mkuu wa Baraza la maaskofu. Waliokuwa ndani ya Kanisa wanajua mambo makubwa ya maendeleo aliyoyaleta ndani ya Kanisa. Hiyo ni sababu mojawapo, pamoja na Dr Slaa kuuacha upadre, hutamsikia padre yeyote au askofu akatamka lolote lenye kudharau mchango wa Dr. Slaa katika Kanisa.

Alipouacha upadre, hakwenda kukaa tu, kama raia wa kawaida alifanya kazi kubwa kwa kushirikiana na wananchi wa karatu katika miradi ya maji ili kuondosha tatizo la maji, ambalo lilikuwa ni tatizo kubwa kwa wilaya ya karatu. Wananchi wakamtaka awe mbunge wao.

Alipoingia bungeni na kupata platform ya kuongelea, ndiye aliyeisema wazi bila woga kashfa ya EPA, na kuwataja viongozi mafisadi. Akiwa M/Kiti wa kamati ya Bunge ya Serikali za mitaa, ni chini ya Dr. Slaa utaratibu wa ukaguzi wa matumizi ya pesa ulibadilika kutoka ukaaji mzuri wa mahesbu ya kihasibu mpaka 'value for money'.

Alipopewa na nafasi ya kugombea nafasi ya Urais alileta changamoto kubwa kwa wagombea wa CCM kiasi cha kufanya idadi ya wabunge wa CDM iongezeke maradufu na kuifanya CDM kuwa chama pinzani kiongozi Bungeni na nje ya Bunge.

Vigezo na mambo aliyoyafanya Dr Slaa ndiyo ishara ya kiongozi bora. Kiongozi bora na makini ana sifa moja kubwa, mahali popote utakapomweka, yeye ataonekana tofauti na wenzake. Hata ukimwambia afanye kazi ya ufagizi, eneo lake litakuwa safi kuliko ya wenzake.

Magufuli
Katika CCM angalao Magufuli ana sifa za kiuongozi. Kwenye ujenzi wa barabara, alipokuwa Shukuru Kawambwa (an example of poorest performers), km 1 ya barabara iligharimu TZS 1.2 billion na miradi ilisinzia sana. Magufuli alipoingia km 1 ikawa TZS 800 milioni na kazi zilienda kasi zaidi. Magufuli alipoenda samaki, wavuvi waliokuwa wakifanya uvuvi haramu walichemka kwelikweli.

Wanachama wa CCM waitazame Tanzania kwa jicho la utaifa, uzalendo na huruma. Wagombea wote waliojitokeza, hakuna mwenye kuleta kitu cha pekee. Wote, bila ya kuvutwa na hisia za kiitikadi tumchague Dr Slaa, mtu mwenye historia ya kuleta mabadiliko kila alipoenda, aibadilishe Tanzania na atuwekee msingi wa Taifa jipya kama alivyofanya George Washington kule Marekani. Ni rahisi sana kuiongoza nchi ambayo tayari misingi yake ipo. Tanzania ya sasa haina misingi imara ya kimfumo na kisheria inayomlazimisha kiongozi yeyote mahali popote alazimike kuwa mwadilifu na mbunifu. Ni lazima tutoke kwenye uongozi wa zawadi, hisani, shukrani na mazoea tuende kwenye uongozi unaozingatia tija (quality and perfection).
 

Lowasa hatakatwa jina kabisa ni kuwa hatachaguliwa na wajumbe wengi.
 
Kuhusu Membe, ni yuleyule kimvuli cha JK, HAFAI KABISA. nchi hii tuendako tunaihitaji mtu strong Nyanja zote, labda Wasira!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…