WamLola
JF-Expert Member
- Aug 12, 2012
- 343
- 122
KWA BARUA HII KWA MWIGULU,UPEPO WA URAIS NDANI YA CCM UMEBADILIKA
Siku kadhaa zilizopita tumeshuhudia Naibu Katibu Mkuu Mwigulu Nchemba akilimwa barua ya kumuamuru kusitisha "harakati" zake za kuzunguka mikoani kwa kofia ya unaibu Waziri na Unaibu Katibu Mkuu kujijenga kwa ajili ya mbio za Urais 2015.
Harakati zake zilihusisha matumizi ya chopa isiyokuwa na baraka za chama,mikutano yake iliibua hisia hasi na hali ya kutotambuliwa kwa viongozi wa kamati za siasa za mkoa,wilaya,kata na hata vijiji,kiufupi Mwigulu alivamia mikoa,Wilaya,Kata na Vijiji bila ruhusa maalumu toka kwa viongozi wa maeneo husika.Hali hii ilijenga mauzi na hasira kwa viongozi wengi wa kamati za siasa na kulifikisha swala hili kwa Kamaradi Kinana,ambaye bila woga alimuonya kwa maneno Mwigulu Nchemba,hata baada ya kukaidi na kuendelea na safari zake alipokea barua kali iliyoamuru asitishe hizo kampeni zake za urais kabla ya wakati.
Kwa sasa Mwigulu si sehemu ya watarajiwa wa ugombea urais ndani ya chama,harakati zake zimetulizwa kwa utovu wake wa nidhamu wa kutokumsikiliza katibu Mkuu ambaye ndiye Mtendaji Mkuu na boss wake ndani ya chama,utovu huu wa nidhamu wa Mwigulu kwa katibu Mkuu wake ni kigezo tosha cha kumuweka pembeni wakati ukifika.Huyu tunamwondoa kwa sasa katika list.
Lazaro Nyalandu,huyu ni "checkbob" tu,anayejitangaza kugombea urais ili nyota yake ya kisiasa isififie,hana uzito wowote na hata kauli yake ya kuutaka urais haikupewa uzito.Huyu anaamini Wamarekani wake alioishi nao ndio watampa urais.
Makamba Jnr hoja yake ilikuwa moja tu,ujana au umri,amepima upepo akakuta hoja hiyo haina mashiko,akaamua kuja kivingine..akajichimbia akaja na kitabu.analazimisha tukisome kwa kununua kurasa za magazeti na kukichapisha kama "Toleo Maalumu",kwa hali ndani ya chama kwa sasa,na upepo wa siasa za kitaifa,Makamba Jnr sio "candidate" mujarabu,labda ajijenge kwa msimu mwingine.
Hali iko hivyo kwa Bernard Membe,kada asiye na ushawishi ndani ya chama,sehemu ya watu wake wamekimbilia kambi ya "Team Sukari,Team asali"...Membe anatajwa kuwa mjivuni na nwenye maringo,anayeamini ameshakuwa rais hata kabla ya kuteuliwa na chama..kambi yake imevurugika na kutawanyika.Inaitaji mujiza kwa Membe kukubalika ndani ya chama,maana kwa CCM hachaguliwi Rais tu,bali mwenyekiti wa chama pia.Hulka ya Membe na ushawishi wake haumpi nafasi ya kupeperusha bendera hiyo,huyu anapewa lkn nafasi ya kuleta upinzani kwa Magwiji wa Chama kama Steven Wassira,Mizengo Pinda na Edward Lowassa.Tuisubiri May itatupa majibu
Edward Lowassa,huyu anatajwa kama kampeni zake zimelalia kwenye pesa,anamwaga pesa kama njugu,Kitengo cha Usalama ndani ya chama kinaendelea kukusanya ushahidi ndani ya harakati na kambi yake,ili wakati ukifika ziwekwe wazi na wanachama waamue,huyu anautaka urais kwa namna zote,ana kambi iliyotawanyika lkn unayofanya kazi kwa msukumo wa pesa na si mapenzi ya dhati kwa mgombea wao,hali yake ya afya pia imekuwa kikwazo,Wengi wa wanakambi wake wanapata wasiwasi juu ya afya yake,ukipata nafasi ya kuwa naye karibu wanakiri kuwa afya yake haiwezi mitikisiko.Siri zao zinavuja kwa sababu walioko huko wengi ni maslahi ya pesa,kambi yake inatumia nguvu kumsafisha na kashfa ya ufisadi.Upinzani wako kimyaa kwa Lowasa sabb wanaamini CCM ikimpitisha kwao itakuwa njia rahisi kuibomoa CCM kwa rekodi ya Lowassa huko nyuma.
Mizengo Pinda ...huyu kaibuka ghafla kama moto wa kifuu,hakuwa na ndoto hizo mpaka aliposhawishiwa na wapambe.Anahitaji nguvu Sana kueleweka kuwa Rais na Mwenyekiti wa CCM,hana ushawishi Mkubwa ndani ya chama,mpole,regerege na asiye mkali hata kwa walio chini yake,katika swala la Escrow hakusiikika kutoa kauli ya kiuongozi na kurudisha imani ya serikali na chama,kauli ya kukemea aliyoitoa Wasira bungeni wakati wa mjadala wa Escrow ilipaswa kutolewa na PM,walau Prof Mwandosya naye alionyesha uhai.CCM na wanachama wake hawatakuwa tayari kuongozwa na Mwenyekiti aina ya Pinda,huyu naye tumpe mda anaweza kutoa upinzani kwa Wassira na Lowassa.
Steven Masatu Wassira,huyu anatajwa na wanaCCM wengi kutaka kugombea urais,anaaminika ktk ujenzi wa hoja,kusimamia ukweli na kile anachokiamini,Alipita kwa kishindo mwaka 2012 katika uchaguzi ndani ya chama.Wanachama wengi wanamsifu kwa kujitoa muhanga ktk midahalo iliyowatisha wengi ndani ya CCM,alihudhuria na kubadili kabisa upepo.Anatajwa kuwa muadilifu asiye na kashfa za ufisadi na ubadhilifu wa Mali za umma.Kauli yake ndani ya Bunge juu ya sakata la Escrow ilifungua ukurasa Mpya kuwa ndani ya CCM kuna watu kama Wassira na Mwandosya wanaotaka wezi hao wawajibishwe,Katika harakati hizi za mabadiliko ya siasa ndani ya nchi,CCM wanaamini kuwa na mtu mwenye uwezo wa kujenga hoja,muadilifu na mwenye maono ya kiuongozi.Wapinzani wake wanatumia turufu ya yeye kuhama chama 1995 baada ya kufanyiwa zengwe ndani ya CCM,Sokomoko la nyumba ya bodi ya sukari iliyoanzishwa na wapinzani wake imeyeyuka,maana amerudishwa tena Wizara ya Kilimo na Chakula ambayo bodi ya sukari i chini yake.Huyu anapewa nafasi kubwa sanaa kutoana jasho na Lowassa,Membe na Mizengo Pinda,kinachowapa ugumu wapinzani wake ni kutokujuwa kambi yake imekaaje.
May hiyo ndio inakuja...Historia iandikwe...Kwa sasa CCM inahitaji mtu muadilifu,mwenye maono na mchapakazi.