Wagombea CCM wajawa hofu Mwanza | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wagombea CCM wajawa hofu Mwanza

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Sep 17, 2012.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Sep 17, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  [h=2][/h]JUMATATU, SEPTEMBA 17, 2012 05:49 NA JOHN MADUHU, MWANZA

  WAKATI vikao vya Chama Cha Mapinduzi (CCM) vinatarajiwa kuanza leo, hofu imetanda miongoni mwa wagombea wa nafasi mbalimbali za chama hicho katika ngazi za wilaya na mkoa.

  Hofu hiyo imetokana na kuwapo kwa makundi yanayotofautiana ndani ya chama hicho, huku kila kundi likijitahidi kujenga ngome yake kwa wafuasi wao kuhakikisha wanapitishwa katika vikao vya juu na hatimaye waweze kuwania nafasi walizoomba.

  Vikao hivyo vinatarajiwa kuanza kwa sekretarieti ya chama hicho kuketi kupitia majina ya wagombea walioomba nafasi za Ujumbe wa Halmashauri Kuu (NEC), uenyekiti wa wilaya na mkoa.

  Kikao hicho cha sekretarieti kitafuatiwa na kikao cha Kamati Kuu na baadhi ya waliokuwa wagombea wa nafasi mbalimbali, walioenguliwa katika vikao vya wilaya na mkoa kwa kupewa alama wanazozilalamikia tayari wamekata rufaa katika ngazi za juu za chama hicho.

  Wanachama wa chama hicho waliojaziwa alama za chini wamekuwa wakilalamika kuwa, taratibu katika baadhi ya vikao zilikiukwa kutokana na misingi ya makundi pamoja na chuki binafsi na kuvitaka vikao hivyo kurejesha majina yao.

  Aliyekuwa mgombea nafasi ya Uenyekiti wa CCM Wilaya ya Ilemela, Richard Rukambura, tayari amewasilisha malalamiko yake katika vikao vya juu, kwa maelezo jina lake lilijaziwa alama za chini katika ngazi ya mkoa na kumuengua katika mapendekezo yake licha ya wilaya kumuona ana sifa.

  “Nimeamua kukata rufaa kwa kuwasilisha malalamiko yangu kwa Kamati Kuu, kutokana na namna chuki zilivyotawala katika kutoa mapendekezo ngazi ya mkoa, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mwanza ndiye chanzo cha malalamiko ya wagombea wengi walioenguliwa kutokana na kukiyumbisha chama chetu.

  “Kama suala ni tuhuma mbona Mwenyekiti wa CCM Mkoa ana tuhuma mbalimbali, zikiwa ni pamoja na kunyang’anya wananchi mashamba, lakini kwa mshangao wa wengi aliamua kujipendelea kwa kushawishi wajumbe kumjazia alama za juu ambazo hastahili.

  “Ila sisi wengine tusio na sauti hatukupendekezwa hivyo Kamati Kuu inapaswa kutengua mapendekezo ya wagombea wa nafasi mbalimbali,” alisema Rukambura.

  Naye, James Bwire, aliyekuwa akiwania nafasi ya ujumbe wa NEC Wilaya ya Nyamagana, alisema ameamua kukata rufaa kutokana na jina lake kuenguliwa katika ngazi ya mkoa, licha ya kupewa alama za juu katika vikao vya chini.

  Mmoja wa wabunge wa zamani wa chama hicho aliyepewa alama za chini kuanzia ngazi za wilaya na mkoa, alisema alipewa alama hizo kutokana na fitina ya kundi moja linaloongozwa na mmoja wa wabunge pamoja na viongozi wa wilaya na mkoa kwa maslahi binafsi.

  “Nimekuwa mbunge kwa miaka 10, pia nimeshika nyadhifa mbalimbali, leo hii ninapewa alama D kwa kosa lipi, CCM isipokuwa makini kupitia vikao vyake vya ngazi za juu, itakwenda kuangamia kwa kuwa sasa inaongozwa kwa chuki.

  “Kuna wagombea ambao wana uwezo mkubwa walienguliwa katika ngazi za wilaya, pia kuna wagombea ambao wana uwezo mdogo na hawana uzoefu ndani ya chama, ila kwa kuwa wako kwa maslahi ya viongozi wamerejeshwa kwa kupendekezwa, vikao vya mkoa si msahafu ndio maana suala hili la madudu ya CCM mkoa tumeamua kulifikisha katika vikao vya juu,” alisema kwa sharti la kutotajwa jina.

   
 2. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #2
  Sep 17, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Pole Diallo... TV yako ilikuwa inampiga chini Mpinzani wako ambaye pia ni Mbunge wa Zamani na Waziri

  Mwanza siasa ni mbaya... What goes around comes around...
   
 3. Mvaa Tai

  Mvaa Tai JF-Expert Member

  #3
  Sep 17, 2012
  Joined: Aug 11, 2009
  Messages: 6,174
  Likes Received: 2,175
  Trophy Points: 280
  Sikio la kufa halisikii dawa, CCM kifo kimewadia hivi ni vimaradhi nyemelezi tuu vitakavyochangia kifo chake.
   
 4. Uhalisia Jr

  Uhalisia Jr Senior Member

  #4
  Sep 17, 2012
  Joined: Sep 10, 2012
  Messages: 134
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hofu tu ndo inaumiza vichwa
   
 5. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #5
  Sep 17, 2012
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,801
  Trophy Points: 280
  Kama dialo anaweza fikishiwa ujumbe huu itakuwa vema!

  HAMIA CHADEMA.
  hutahitaji kuhonga hata senti kipande kuomba nafasi ya kuongoza, hutapata hasara ukichaguliwa ama usipochaguliwa. Na TV station yako itaandikwa kuwa ilichangia kumfurusha mkoloni mweusi CCM.
   
 6. Lyimo

  Lyimo JF-Expert Member

  #6
  Sep 17, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 3,828
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Hawa CDM ni wakorofi sana, yani wamewapa alama za chini washindani wenye uwezo na kuwapa za juu wale wasio na uwezo. CDM sasa wanafanya hata chama chetu CCM kisitawalike, tunakuelekeza Tendwa uwafutie usajili hawa CDM.
   
 7. PPM

  PPM JF-Expert Member

  #7
  Sep 17, 2012
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 839
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Masha yuko uko? au bado yuko RG anachangisha mchango wa harusi ya Mlatie
   
 8. k

  kimeloki JF-Expert Member

  #8
  Sep 17, 2012
  Joined: Jul 9, 2012
  Messages: 1,927
  Likes Received: 950
  Trophy Points: 280
  vurumisha chama cha maulaji! vurumishaaaaaaaaaaaaa!!!!!
   
 9. Maarko

  Maarko JF-Expert Member

  #9
  Sep 17, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 1,030
  Likes Received: 189
  Trophy Points: 160
  "Mungu akitaka kumuangamiza mtu humpofusha asione kitakacho mkuta mbeleni"Mh Samwel Sitta.
  Aliyaongea hayo wakati wa uchaguzi mkuu wa mwaka 2010,hayo ndiyo yanayoikuta ccm,utawala wa ccm umefitinika wenyewe kwa wenyewe wanamalizana!
   
 10. sir.JAPHET

  sir.JAPHET JF-Expert Member

  #10
  Sep 17, 2012
  Joined: May 18, 2012
  Messages: 700
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Jumatatu, Septemba 17, 2012 05:49 Na John Maduhu, Mwanza WAKATI vikao vya Chama Cha Mapinduzi (CCM) vinatarajiwa kuanza leo, hofu imetanda miongoni mwa wagombea wa nafasi mbalimbali za chama hicho katika ngazi za wilaya na mkoa. Hofu hiyo imetokana na kuwapo kwa makundi yanayotofautiana ndani ya chama hicho, huku kila kundi likijitahidi kujenga ngome yake kwa wafuasi wao kuhakikisha wanapitishwa katika vikao vya juu na hatimaye waweze kuwania nafasi walizoomba. Vikao hivyo vinatarajiwa kuanza kwa sekretarieti ya chama hicho kuketi kupitia majina ya wagombea walioomba nafasi za Ujumbe wa Halmashauri Kuu (NEC), uenyekiti wa wilaya na mkoa. Kikao hicho cha sekretarieti kitafuatiwa na kikao cha Kamati Kuu na baadhi ya waliokuwa wagombea wa nafasi mbalimbali, walioenguliwa katika vikao vya wilaya na mkoa kwa kupewa alama wanazozilalamikia tayari wamekata rufaa katika ngazi za juu za chama hicho. Wanachama wa chama hicho waliojaziwa alama za chini wamekuwa wakilalamika kuwa, taratibu katika baadhi ya vikao zilikiukwa kutokana na misingi ya makundi pamoja na chuki binafsi na kuvitaka vikao hivyo kurejesha majina yao. Aliyekuwa mgombea nafasi ya Uenyekiti wa CCM Wilaya ya Ilemela, Richard Rukambura, tayari amewasilisha malalamiko yake katika vikao vya juu, kwa maelezo jina lake lilijaziwa alama za chini katika ngazi ya mkoa na kumuengua katika mapendekezo yake licha ya wilaya kumuona ana sifa. “Nimeamua kukata rufaa kwa kuwasilisha malalamiko yangu kwa Kamati Kuu, kutokana na namna chuki zilivyotawala katika kutoa mapendekezo ngazi ya mkoa, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mwanza ndiye chanzo cha malalamiko ya wagombea wengi walioenguliwa kutokana na kukiyumbisha chama chetu. “Kama suala ni tuhuma mbona Mwenyekiti wa CCM Mkoa ana tuhuma mbalimbali, zikiwa ni pamoja na kunyang’anya wananchi mashamba, lakini kwa mshangao wa wengi aliamua kujipendelea kwa kushawishi wajumbe kumjazia alama za juu ambazo hastahili. “Ila sisi wengine tusio na sauti hatukupendekezwa hivyo Kamati Kuu inapaswa kutengua mapendekezo ya wagombea wa nafasi mbalimbali,” alisema Rukambura. Naye, James Bwire, aliyekuwa akiwania nafasi ya ujumbe wa NEC Wilaya ya Nyamagana, alisema ameamua kukata rufaa kutokana na jina lake kuenguliwa katika ngazi ya mkoa, licha ya kupewa alama za juu katika vikao vya chini. Mmoja wa wabunge wa zamani wa chama hicho aliyepewa alama za chini kuanzia ngazi za wilaya na mkoa, alisema alipewa alama hizo kutokana na fitina ya kundi moja linaloongozwa na mmoja wa wabunge pamoja na viongozi wa wilaya na mkoa kwa maslahi binafsi. “Nimekuwa mbunge kwa miaka 10, pia nimeshika nyadhifa mbalimbali, leo hii ninapewa alama D kwa kosa lipi, CCM isipokuwa makini kupitia vikao vyake vya ngazi za juu, itakwenda kuangamia kwa kuwa sasa inaongozwa kwa chuki. “Kuna wagombea ambao wana uwezo mkubwa walienguliwa katika ngazi za wilaya, pia kuna wagombea ambao wana uwezo mdogo na hawana uzoefu ndani ya chama, ila kwa kuwa wako kwa maslahi ya viongozi wamerejeshwa kwa kupendekezwa, vikao vya mkoa si msahafu ndio maana suala hili la madudu ya CCM mkoa tumeamua kulifikisha katika vikao vya juu,” alisema kwa sharti la kutotajwa jina. Toa Maoni yako kwa habari hii
   
Loading...