Wafungwa 42 wafaulu mtihani darasa la saba

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
74,627
154,986
KAMPALA,Uganda

WAFUNGWA 42 waliofanya mtihani wa darasa la saba mwaka jana katika gereza la Luzira nchini Uganda wamefaulu masomo yao ya kujiunga na Sekondari.

Habari zilieleza kutoka Kampala jana kuwa kati ya wafungwa hao 42, watatu kati yao wamefaulu kwa kiwango cha daraja la kwanza, 17 kiwango cha daraja la pili, 13 daraja la tatu, huku wafungwa wengine nane wakifaulu kiwango cha daraja la nne.


Ilielezwa, mwanafunzi ambaye alifanya vizuri zaidi ni Bw. Aziz Bogere ambaye amefaulu kwa kiwango cha daraja la kwanza na pointi 11.

Wafungwa wengine waliofaulu kwa daraja la kwanza wametajwa kuwa ni Bw. Godfrey Tabu na Bw. Ronald Ssenyange ambao wamefaulu kwa kiwango cha alama ya pointi 12.

Ofisa mwandamizi wa Ustawi wa Jamii ambaye pia ndiye Mwalimu Mkuu,Bw. Anatoli Biryomumaisho alisema kuwa matokeo ya mwaka huu yameongezeka ikilinganishwa na matokeo ya miaka ya nyuma.


"Mwaka 2008,tulikuwa na mfungwa mmoja tu aliyefaulu kwa kiwango cha daraja la kwanza,"alisema Bw. Biryomumaisho.

"Hatujawahi kupokea fedha za mpango wa kutoa elimu kwa wafungwa .Hatuna vifaa vya kufundishia bali tumekuwa tukiwatumia wafungwa ili wakawafundishe wenzao na vilevile hatuna walimu wenye mafunzo,"aliongeza Bw. Biryomumaisho na akaiomba Wizara ya Elimu kuwapatia vifaa muhimu vya kufundishia.



Alisema kuwa endapo wataingizwa katika mpango huo wa wa Serikali wa kupatiwa fedha kwa ajili ya mafunzo ana imani kuwa ufaulu wao utaongezeka hadi kuzipita shule nyingine zilizopo katika mazingira mazuri.

Bw. Biryomumaisho alisema kuwa elimu ndiyo ufunguo muhimu wa kuwapa mabadiliko na raslimali wafungwa huku akisema kuwa wafungwa wengi wameonekana kuwa na nia ya kupata elimu hiyo.

"Tuna wafungwa wapatao 800 ambao wapo katika mapngo wa elimu ya msingi na tuna amini kuwa idadi hiyo inaweza kuongezeka zaidi,"alisema Bw.Biryomumaisho.(New Vision)
 
Back
Top Bottom