Wafugaji wa kuku naomba msaada wenu

Wafugaji wa kuku naomba msaada wenu

hps300

Senior Member
Joined
Feb 20, 2016
Posts
170
Reaction score
152
Wana bodi nianze kwa kutoa pongezi kwa michango mbalimbali ambayo mmekuwa mkiiweka hapa jukwaani. Baada ya kupitia hili jukwaa la kilimo na ufugaji kwa kipindi kirefu nami nilishawishika kujaribu ufugaji wa kuku chotara, Nilianza mradi huu kama majaribio kwanza kabla sijaingia rasmi.

Nilianza kwa kununua mayai trei 4 ambazo zina jumla ya mayai 120. Baada ya siku 21 nilifanikiwa kupata vifaranga 101. Ambao niliwalea, wakiwa kwenye brooder 7 walifariki wakabaki 94. Baada ya miezi 2 niliwaamishia bandani.

siku ya kwanza tu bandani usiku akaingia mnyama ambaye kazi yake ilikuwa ni kukatata vichwa tu na kuacha. aliua kama vifaranga 19 hivi. Nilijaribu kuchunguza banda na nikagundua wapi alipitia na nikafanikiwa kupaziba. Kwa kiasi fulani nilifanikiwa na kuku wakakuwa na kuanza kutaga.

Wakiwa kwenye peak ambapo atleast kwa siku nilikuwa napata trei 3 na zaidi, kuku wakaanza kuugua. Tatizo hili linawakabili majike tu majogoo hawajaguswa hata mmoja. TATIZO LENYEWE KUKU WANAHARISHA MAJI KABISA wakati mwingine yanakuwa na weupe.

Kiasi inafikia mpaka kuku analowana kabisa upande wa nyuma. nilijaribu kumchinja kuku na kumpeleka kwa Vet mmoja akanambia huo ni Mdondo, Lakini pia ukimchinja kuku anakuwa na harufu kali sana tumboni, Cha kushangaza ilikuwa ni mwezi mmoja tu tangu niwape chanjo, na nimejitahidi kufuatilia chanjo kiasi sipitishi hata siku moja.

Hivi ninavooandika kati ya mitetea 50 wamebaki 11 na majogoo wapo wote 13. Swali kama tatizo ni mdondo kwa nini wanakufa tu majike na si majogoo.
Hebu wazoefu tusaidiane hapa.

Natanguliza shukrani.
 
awali yayote nikupe hongera kwa kukubali.changamoto na kusimama tena weng huairisha kabisa, sasa hapo nashaa kitu ki1 mdondo haubagui jinsia ya kuku.
hivyo napata hofu kumwamin mtaalam huyo hembu badili mtaalam alafu tatizo watalam wengi wameishia kusoma notes2 hembu tembelea wafugaji zaid kuliko wataalam
 
Asante kwa ushauri najipanga kufanya hivo
 
Hawa kuku chotara ndio hao wa naitwa kuloirer ambao kila mahali wanatangazwa
 
Back
Top Bottom