Wafuasi CHADEMA,CCM watwangana Songea | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wafuasi CHADEMA,CCM watwangana Songea

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by mgomba101, Oct 21, 2012.

 1. m

  mgomba101 JF-Expert Member

  #1
  Oct 21, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 1,788
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  SIKU chache mara baada ya kuanza kwa kampeni za uchaguzi mdogo wa madiwani wa Kata ya Mpepai iliyopo wilayani Mbinga na Mletele wilayani Songea mkoani Ruvuma zikiwa zimeanza, wafuasi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wamefanyiana fujo zilizosababisha baadhi kujeruhiwa.

  Katika vurugu hizo ambazo pia zimesababisha gari moja la CCM kuvunjwa kioo zilishuhudiwa na Mwenyekiti wa chama hicho Mkoa wa Ruvuma Oddo Mwisho na Katibu wa chama hicho Wilaya ya Mbinga, Anastazia Amasi, wote wakiwa ndani ya gari hilo.

  Viongozi hao na wafuasi wa chama hicho walikuwa wakitoka kwenye mkutano wa kampeni katika eneo hilo ghafla walikuta kundi la wanawake wanaodaiwa kuwa ni wafuasi wa CHADEMA wakiwa wamelala barabarani kuzuia msafara huo na baada ya kusimama ndipo gari hilo lilipoanza kushambuliwa kwa mawe na katika jitihada za kujiokoa Mwenyekiti Oddo Mwisho alifanikiwa kukimbia akimuacha Katibu Anastazia Amasi akishambuliwa na kundi hilo ambalo lilifanikiwa kuvunja kioo cha gari.

  Akizungumzia tukio hilo, Katibu wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Ruvuma, Velena Shumbusho alisema kuwa tukio hilo la vyama hivyo viwili vyote vilikuwa vinatoka kwenye ufunguzi wa kampeni za uchaguzi mdogo wa Kata ya Mpepai wilayani Mbinga na vurugu zilizuka wakati wafuasi wa CCM wakiwa wanarudi.

  Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Mbinga, Senyi Ngaga, alipoulizwa kuhusiana na tukio hilo alikiri kutokea, hata hivyo alisema hawezi kusema kuwa waliohusika na vitendo hivyo ni wafuasi wa CHADEMA kwani uchunguzi bado unaendelea kwa lengo la kuwabaini wahusika.

  Mpaka sasa hakuna mtu yeyote aliyekamatwa kuhusiana na tukio hilo na uchunguzi bado unaendelea ili wahusika watakapobainika sheria iweze kufuata mkondo wake.
   
 2. Nicole

  Nicole JF-Expert Member

  #2
  Oct 21, 2012
  Joined: Sep 7, 2012
  Messages: 4,284
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Hizi siasa zimefika huko?kwanini wasishambuliane kwa hoja na mwisho wa mchezo sanduku la kura lifanye maamuzi?hizo ni akili za viroba2.
   
 3. Miwatamu

  Miwatamu JF-Expert Member

  #3
  Oct 21, 2012
  Joined: Oct 2, 2012
  Messages: 1,453
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 133

  Binafsi sielewi hawa watu wanakuwa na lengo gani! Hebu tujaribu kwa wastaarabu wa kupingana kwa hoja bwana.....! kwangu inakela sana hali hii.
   
Loading...