beth
JF-Expert Member
- Aug 19, 2012
- 3,879
- 6,356
Watu wawili wakazi wa Manispaa ya Dodoma wamefikishwa katika mahakama ya hakimu mkazi mkoa wa Dodoma kwa tuhuma za mauaji ya Mwanasheria wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mkoa wa Dodoma Emmanuel Meta.
Watuhumiwa hao ni Boniface Mwambene (23) ambaye ni fundi ujenzi na pia ni mkazi wa Ipagala katika manispaa ya Dodoma na Juma Athumani (25) ambaye ni dereva wa bodaboda na pia ni mkazi wa Swaswa katika Manispaa ya Dodoma.
Akisoma mashtaka mbele ya hakimu mkazi wa mahakama ya mkoa wa Dodoma, Elias Anangisye, karani wa mahakama hiyo Stanley Konyanza amesema kuwa watuhumiwa hao walitenda kosa hilo Januari 20 mwaka huu.
Kesi hiyo namba 12 ya mwaka 2016 (PI) imeahirishwa hadi Machi 24 mwaka huu itakapotajwa tena na washtakiwa hawakutakiwa kujibu kitu chochote kwa kuwa mahakama hiyo haina uwezo wa kusikiliza kesi za mauaji.
Washtakiwa hao wamerudishwa rumande.
Mwanasheria huyo wa Takukuru mkoa wa Dodoma, aliuawa kwa kupigwa na vitu vizito vilivyosababisha kuvuja damu nyingi na alifariki dunia wakati akipatiwa matibabu kwenye hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma.