Wafanyakazi wa Tanzania wanafanya kazi kwa hofu

Nkungulume

JF-Expert Member
Nov 25, 2015
2,987
1,209
Wakuu kwa kipindi hiki cha uongozi wa serikali ya awamu ya tano kumekuwa na tatizo kubwa la wafanyakazi wa taasisi za uma na mashirika ya uma kufanya kazi kwa hofu kubwa.

Hii imetokana na aina ya uongozi wa Dr. JPM na jopo lake kuona kuwa kutumbua majipu ndiyo aina bora ya uongozi.

Maana sasa waziri kama hajamfukuza kazi kiongozi katika taasisi yake anaonekana kama vile hawajibiki mtindo huu siyo mzuri maana umesababisha wafanyakazi wengi.
kukata tamaa na kuvunjika moyo na wengine kufanya kazi kwa hofu kubwa.

Nadhani ni wakati sasa wa serikali kujipanga upya na kuona namna bora ya kuoongoza maana bila ya kuwa waangalifu watafukuzwa wafanyakazi bora kwa majungu au chuki binafi za ulipizaji kisasi.

Magufuli kuwa makini sana na jambo hili.
 
Kama wewe ni jipu utafanya kazi kwa hofu lakini kama unajiamini na kazi yako huwezi kuhofu lolote.
 
Back
Top Bottom