Wafanyakazi wa serikali nani atatusaidia?

lopinavir

Senior Member
Jul 11, 2015
186
121
Baada ya taarifa kwa watumishi wa umma kutoka utumishi kuwa utaratibu wa mishahara sasa kulipwa kutoka benki kuu kumekuwa na mkanganyiko mkubwa kwa watumishi hawa.
-imetakiwa taarifa za kibenki za mtumishi zifannane na za kwenye payroll,hapa ndipo tatizo lilipo haswa:
-Unakuta mtu anaitwa,mfano(Hamisi Ally Chacha),ambalo ndiyo jina lake sahihi.
-Ndilo jina lililopo bank,lakini kwenye payroll unakuta wakati wanaingiza jina lake likaandikwa Hamis Ally Chacha(HAMIS-HAWAKUANDIKA "I" MWISHONI)
-Mtumishi huyu ataambiwa jina lake ni tofauti hivyo anapaswa kusahihisha jina lake na wanasema kwenye payroll huwezi kubadili jina,inabidi ubadili taarifa za kibenki(hapa ndipo usumbufu ulipo)
-Utaratibu wa kubadili taarifa za kibenki ili ziendane na zile za kwenye payroll ukawa ni kuchukua barua ya kumtambulisha mfanyakazi kutoka kwa afisa utumishi,unaenda nayo banki(CRDB) wanakupa form ya kumtambulisha huyo mtumishi mtaani kwake,ile form ikajazwe na afisa mtendaji then inafunguliwa account nyingine.
-Akaunti iliyokuwepo wanakwambia haitatumika Kuanzia Julai kwa ajili ya mshahara, then wanakwambia uandike barua kwa mwajili wako kuhusu kubadili akaunti ya mshahara(kutoka kwenye akaunt xxxxx yenye jina Hamisi Ally Chacha kwenda kwenye akaunti xxxx yenye jina Hamis Ally Chacha)
-Kuanzia 24/5/17 benki(CRDB) wamekuja na utaratibu mwingine tena kwamba katika hayo yote mtumishi anayotakiwa kufanya anapaswa kwenda mahakamani kuchukua affidavit ya kiapo ili kiambatanishwe kwenye hayo maombi ya kufungua akaunti nyingine.


Swali langu: kama makosa walifanya benki katika kuandika jina langu au makosa walifanya utumishi katika kuandika jina langu,kwa nini mtumishi ndo asumbuliwe kufanya hayo yote,kwa nini wasiwajibike waliokosea?

-Kama natakiwa kufungua akaunti nyingine yenye jina linaloendana na lile ya kwenye saraly slip yangu na mwajili wangu nikamnotify kuwa nimebadili akaunti,kwanini niende mahakamani tena kula kiapo cha kulikana jina langu sahihi na ni kwa makosa yaliyofanywa na utumishi au banki(CRDB) wenyewe?

Nawasilisha...
 
Kwa kweli hapo mtu pekee anaeweza kutusaidia kwa hilo mimi hata simuoni.
 
Hakuna ubishi wala malumbano kuhusu hilo la mishihara kulipiwa kupitia BOT zaidi ya kufuata maagizo na maelekezo utakayopata ili kuondoa utata wa majina yaliyotofauti kati ya account na payroll.
 
Pole sana kwa unayoyapitia...Uzembe wa watu fulani ndio unakuharibia mambo yako aseeh
 
  • Thanks
Reactions: SDG
Magufuli anataka kuwalipa watu aliowahakiki tu waiokwepa kupeleka vyeti itakula kwao
 
Magufuli anataka kuwalipa watu aliowahakiki tu waiokwepa kupeleka vyeti itakula kwao
Hapa si swala la uhakiki,hapa ni swala la usumbufu, maana kama kuhakiki wameshahakiki....
 
Jibu ni rahisi tu "serikali haiwahitaji ndiyo maana inafanya kila namna mkate tamaa mtoke lakini mmeng'ang'ania kama kupe" tokeni njooni tulime huku wabaki wafuatao wanaohitajika huko: Bashite, Gumbo, Happy na Mnyeti
 
Pumbafu wakati mnfoji vyeti,na mnakula mshahara kiwzi wiz ulituambia ww
Inawezekana vyeti nilivyonavyo hukuwahi na hutakuja kuwa navyo wewe wala ndugu yako wala ukoo wako wote...!!kama kitu hujui ni Bora ukanyamaza...!!ukibisha weka vyeti vyako hapa na mimi niweke vya kwangu...
 
Jibu ni rahisi tu "serikali haiwahitaji ndiyo maana inafanya kila namna mkate tamaa mtoke lakini mmeng'ang'ania kama kupe" tokeni njooni tulime huku wabaki wafuatao wanaohitajika huko: Bashite, Gumbo, Happy na Mnyeti
Inawezekana wote nchi hii kuingia kwenye kilimo,sawa,huduma nyingine tutahudumiwa na nani?ukienda hospitali unataka huduma,nani ataitoa na wote tupo shambani?tunachopaswa kujua ni kwamba,kila mmoja anamtegemea mwingine kwa namna ya tofauti
 
Inawezekana wote nchi hii kuingia kwenye kilimo,sawa,huduma nyingine tutahudumiwa na nani?ukienda hospitali unataka huduma,nani ataitoa na wote tupo shambani?tunachopaswa kujua ni kwamba,kila mmoja anamtegemea mwingine kwa namna ya tofauti
Nimekutajia wanaotakiwa kubaki
 
Acha kazi za kuajiriwa kama utaki usumbufu kaji ajiri ila kama bado mme ajiriwa fata mashariti na vigezo vya boss ukienda kinyume na bos huna kazi
SIPENDI KUAJILIWA
 
Back
Top Bottom