mwl. mziray
JF-Expert Member
- Jul 12, 2015
- 597
- 398
Habari wana JF,
Kwa muda mrefu nimeshuhudia wafanyakazi wanaoajiriwa na kampuni za ulinzi kulinda ktk taasisi mbalimbali, wakiombaomba fedha kwa wateja wa taasisi hizo.
Kwa mara ya kwanza niliona mchezo huo nikiwa nasoma chuo kimoja pale Dar es salaam maeneo ya Taifa ambapo nilizoea kuona walinzi wakiomba sh.500 au 1000 ya chai kwa wanachuo kila mara.
Mara ya pili nilifika ktk bank ya NMB tawi la Same Kilimanjaro mwezi wa pili kupata huduma za kibank. Nilipokuwa ndani nilipigiwa simu hivyo nikatoka kupokelea simu nje. Baada ya kumaliza maongezi niliona mlinzi akiniita na nilipofika akaniomba sh.1000 ya chai kwamba ana njaa na hana kitu mfukoni japo ilikuwa ni katikati ya mwezi.
Naomba mawazo yenu wana Jf, tatizo hili linachangiwa na nini na athari zake zinaweza kuwa zipi?
Nawasilisha