singidadodoma
JF-Expert Member
- Nov 11, 2013
- 4,394
- 1,536
KATIKA kampeni za uchaguzi mkuu wa mwaka jana, Rais John Magufuli na Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan, waliwaahidi wananchi kuwa Serikali ya Awamu ya Tano, itawatumikia na kujali wananchi wote, hasa wananchi wa kawaida.
Pia, waliahidi kuwa kazi na mipango yote itakayopangwa na kusimamiwa na serikali, itatatua kero mbalimbali za wananchi, itaongoza mabadiliko makubwa ya kiutendaji, kusimamia matumizi ya mali za umma na rasilimali za taifa, na kugawa rasilimali hizo kwa haki.
Rais amekuwa akisisitiza kuwa mambo waliyoyaahidi kwa wananchi, watayatekeleza kwa sababu ahadi ni deni ; na kwamba wananchi wawaamini kuwa hawakutoa ahadi hizo ili tu wawapigie kura, bali kwamba hicho ndicho serikali inachofanya.
Ni dhahiri wananchi wamedhihirisha ukweli wa maneno hayo ya Rais Magufuli, hasa waliposikiliza hotuba yake ya Sherehe za Mei Mosi, zilizofanyika kitaifa mkoani Dodoma.
Katika hotuba hiyo Rais, alifafanua hatua mbalimbali ambazo serikali yake imechukua tayari ; na zile itakayozichukua kuanzia mwaka ujao, kuboresha maisha ya wananchi, wakiwemo wafanyakazi wa kawaida.
Kwa mfano, hatua mojawapo ni kupunguza kodi inayokusanywa na serikali katika mishahara, maarufu kama Pay as You Earn (PAYE) kutoka asilimia 11 hadi asilimia 9 kuanzia mwaka ujao wa fedha wa 2016/17.
Anasema kwa muda mrefu, wafanyakazi wamekuwa wakiomba serikali ipunguze PAYE ; na kwamba sasa serikali imesikia kilio hicho. Hatua hiyo itawapunguzia makato wafanyakazi hao na kuwapa ahueni kubwa.
Kiwango hicho cha PAYE kitakapopunguzwa, kutakuwepo na pengo katika makusanyo ya kodi za serikali, lakini tuna imani serikali hiyo hiyo, itapanua vyanzo vyake vya kodi, kufidia pengo hilo.
Jambo lingine ambalo Rais Magufuli amewaahidi wafanyakazi ni kuwa hapo baadaye serikali itapandisha mishahara, lakini kwamba serikali imeona ianze kwanza na suala hilo la PAYE, ambalo limekuwa likilalamikiwa kwa muda mrefu na watumishi.
Hatua nyingine Rais alibainisha kuwa itawanufaisha watu wa kawaida ni kuendeleza msako wa watumishi hewa ili fedha zitakazookolewa, zitumike kuboresha mishahara. Wapo watumishi wengi wanaofanya kazi kwa bidii na uaminifu wa hali ya juu. Lakini, wapo wachache ambao ni wafanyakazi hewa, ambao wamekuwa wakilipwa mishahara bila kufanya kazi.
Baadhi ya watu hao ama walishakufa, walishafungwa, walishastaafu au wapo masomoni.
Msako wa wafanyakazi hewa unaondelea nchini, umebaini kuwa hadi jana kulikuwa na wafanyakazi hewa 10,295, ambapo 8,000 ni kutoka Serikali za Mitaa na karibu 2,000 wa Serikali Kuu ambao wamekuwa wakilipwa jumla ya Sh bilioni 11 kwa mwezi na kwa mwaka karibu Sh bilioni 139 na kwa miaka mitano Sh bilioni 996.
Ni wazi fedha ambazo zinatumika kulipa watumishi hewa kwa miaka mitano; zinatosha kabisa kujenga daraja la kisasa, kama Daraja la Nyerere, Kigamboni Dar es Salaam lililofunguliwa juzi; au zingeweza kujenga hospitali nyingi na shule nyingi za kisasa.
Kwa hiyo, kinachotakiwa kufanywa kwa sasa ni tuendelee kuwafichua wafanyakazi hewa ; na pia turipoti kwa vyombo vya dola maofisa wote wa serikali, wanaoendelea kuwalipa ili serikali iwachukulie hatua kali.
Jambo la pili ni wafanyazi wote tuiunge mkono Serikali ya Rais Magufuli, kwa kujituma na kuchapa kazi kwa bidii, weledi na uaminifu wa hali ya juu. Mungu Ibariki Afrika. Mungu Ibariki Tanzania.