Wafanyakazi TTCL mbaroni

neema shamuhenya

JF-Expert Member
Joined
May 24, 2018
Posts
312
Reaction score
216
SHIRIKA la Mawasiliano Tanzania (TTCL) limesema, wafanyakazi wake wawili waliokamatwa hawakuiba data au kudukua taarifa za wateja, ila walihujumu malipo yaliyofanywa na wateja wa shirika hilo.

Kwa mujibu wa taarifa ya ofisi ya uhusiano TTCL makao makuu, kumekuwa na taarifa potofu zinazosambazwa na vyanzo mbalimbali vya taarifa.

Jeshi la Polisi katika Kanda Maalumu ya Dar es Salaam limetangaza kuwashikilia wafanyakazi wawili wa TTCL kwa tuhuma za kuhujumu shirika hilo la umma.

Kamanda wa Kanda hiyo, Lazaro Mambosasa amewataja watuhumiwa hao ambao ni Kelvin Siame (25) mkazi wa Tabata Segerea Manispaa ya Ilala ambaye ni mfanyakazi wa Kitengo cha Huduma kwa Wateja na Lilian Hosea (36) mkazi wa Mbezi Beach Manispaa ya Kinondoni ambaye ni mhasibu.

Kamanda Mambosasa amesema watuhumiwa hao walikamatwa Julai 12, mwaka huu baada ya Polisi kupata taarifa kutoka kwa Ofisa Upelelezi wa TTCL kuwa kuna wafanyakazi wanajihusisha na udukuzi wa data za Shirika la TTCL kutoka taasisi za serikali zinazotumia mtandao wa TTCL.

Amezitaja taasisi hizo kuwa ni Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF), Shirika la Nyumba (NHC) na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).

“Taasisi hizi zimekuwa zikinunua data kutoka shirika la mawasiliano la TTCL kwa ajili ya matumizi ya kila siku lakini watuhumiwa hawa wamekuwa wakiiba data hizo na kuwauzia watumiaji binafsi kwa manufaa yao na kulisababishia shirika hasara ya Sh milioni 46,” alisema Kamanda Mambosasa.

Amesema, watuhumiwa hao wamehojiwa na kukiri kushirikiana na baadhi ya mawakala wa TTCL kuuza data ambazo walikuwa wakizidukua kutoka kwenye taasisi hizo. Watafikishwa mahakamani upelelezi utakapokamilika.

Chanzo: Habari leo
 
Angalau hawa wanajua kujiongeza .
Mimi siku hizi nikisikia mtumishi kajiongeza nampongeza. Miaka mitatu mfululizo huongozi mishahara kwa kiburi binafsi ni dharau sana.
 
Hao wanaosambaza taarifa potofu kwanini wasichukuliwe hatua za kisheria
 
Jela hiyooooo "" inawaita " usikute hapo Katika hiyo hasara ya ml.46 wao waliishia kupata ml.5 ..5 .tu..hiyo ni banda ya kupigiana pasu na hao washirika wenzao
 
Asee watu wanajua kujitosa bila woga.
 
Hii inaitwa rudi nyumbani kumenoga kwa Wizi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…