Wafanyakazi Tazara wapinga siku 14 za uongozi

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
219,463
911,172
Wafanyakazi Tazara watoa siku 14 kwa uongozi
Friday, 10 December 2010 21:05

Zaina Malongo



WAFANYAKAZI wa Shirika la Reli Tanzania na Zambia (Tazara), wamepinga siku 14 zilizotolewa na Serikali kushughulikia kero zao kwa kuwa muda huo, ni mrefu.



Wafanyakazi hao, walisema hayo jana baada ya kukutana na uongozi wa shirika hilo, waliutaka uongozi huo, kumuondoa kazini ofisa muajiri ambaye ni raia wa Zambia kwa kuwa ameshindwa kutekeleza majukumu yake.



Wafanyakazi hao, wanalalamikia ofisa huyo kwa kutosikiliza malalamiko yao ya kutopandishiwa mishahara kwa zaidi ya miaka kumi sasa tangu waanze kazi. Wafanyakazi hao, walikutana na uongozi wa shirika hilo, kupinga majibu yaliotolewa na Kaimu Mkurugenzi wa Tazara, Dumas Ndumbaro.

Akizungumza na wafanyakazi hao, Ndumbaro alisema juzi, uongozi wa Tazara ulipokea barua ya malalamiko yao yao na kwamba waliipeleka Wizara ya Uchukuzi kwa ajili ya kupatiwa majibu baada ya siku 14.


“Tatizo ni la muda mrefu, lakini suala la kutaka ofisa rasilimali watu aondolewe kwa mara moja ni vigumu kwa kuwa Tazara inaongozwa na nchi mbili,”alisema Ndumbaro.

Wafanyakazi hao, wakiongozwa na kiongozi wa Umoja wa Wafanyakazi wa Reli nchini (Trawu), Sylivester Rwegasira ambaye aliwauliza wafanyakazi hao, wanasemaje na mmoja wao, Ram Hussein alisema wanachokitaka ni ofisa rasilimali watu kuondolewa kazini.


Naye Teresi Mhalatile alisema wanataka ofisa mwajiri aondolewe kazini kwa sababu amekalia madai yao kwa muda mrefu bila majibu.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Tazara, Mbikusita Lewanika, alituma maelezo ya maandishi kwa gazeti hili kutoka nchini China akieleza kuwa ameunda kamati maalumu ya mameneja na maofisa kushughulikia
suala hilo.



Alisema kamati hiyo, itaongozwa na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji, Dumas Ndumbaro ili kushughulikia matatizo hayo na kwamba itatoa mapendekezo ya kutatua kero mbalimbali, ikiwemo kurekebisha mishahara ya wafanyakazi.
 
Can they sit down and do some work really ? All they want is singing tht mshikamano song, drink some cofee and nothing ever gets done ! There r so many people out there lkng for jobs, public funds @ stake!
 
Back
Top Bottom