Rev. Kishoka
JF-Expert Member
- Mar 7, 2006
- 4,526
- 1,552
Wafanyakazi wa Tanzania na Watanzania wote wenye akili timamu, msiichangie CCM katika kampeni yake ya SMS au namna yeyote ya michango iwe ni matembezi =, karamu au mnada ili ipate pesa za uchaguzi mwaka huu.
Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Tanzania ambaye ndiye mwajiri mkuu, keshajitapa na kuutambia ulimwengu kuwa haitaji kura za wafanyakazi, hivyo hastahili kuchangiwa na mfanyakazi yeyote, iwe ni yeye au chama chake!
Wafanyakazi Msiichangie CCM, haijali Maslahi yenu! Inajijali nafsi yake na ndio maana haioni umuhimu wa kuboresha maisha yenu na ya Watanzania bali ni kudumisha utawala wake kwa udi na vumba!
Kama CCM ingekuwa na niya ya kuleta Maisha bora kwa Watanzania, basi kwa udi na vumba ingehakikisha inafanya hivyo kwa kutetea na kupigania maslahi ya Mtanzania na hata kutafuta mbinu zote kuongeza kipato cha Taifa ili kila Mtanzania anufaike.
Natoa hoja kwako ndugu Mtanzania, kama umelogwa na umepagawa endelea kuamini CCM itakuondolea Ujinga, Umasikini na Maradhi. Mwenyekiti wa CCM kesha sema hadharani hahitaji kura za Watanzania wanaotaabika, endeleeni kutaabika na hajali mtaishije katika umasikini na haelewi kwa nini nyinyi ni masikini.
Kama kura hataki, basi na fedha msimchangie huyu asiye na uungwana!