WAFANYAKAZI HEWA NA WAKUU WA IDARA WASIO NA SIFA

Ng'wanambula

Senior Member
Oct 2, 2011
197
54
Naipongeza sana serikali ya JPM kwa kuangazia tatizo la watumishi hewa ambao kila mwezi wanaigarimu.serikali fedha nyingi. Hata hivyo kuna tatizo ju
Jingine linaloendana na hilo, la wakuu.wa idara wasio na sifa. Hawa huwa wanapewa nafasi hizo kama upendeleo maalum ili kulinda ulaji wa wanaowapa nafasi hizo. Wale wenye sifa stahiki hawapewi nafasi hata kama miongozo inaelekeza hivyo. RAIS AIMULIKE MANISPAA YA SHINYANGA,kuna tatizo hili sana la kupeana vyeo kwa upendeleo. Utakuta mtu ana Diploma anapewa ukuu wa idara huku wenye degree na Masters na uzoefu wa kutosha wakiachwa pamoja na kwamba miongozo iko wazi juu ya sifa za mkuu wa idara. Huo pia ni ufisadi. Chonde chonde JPM tutumbulie hili lipu maana hizi ofisi watu wamegeuza kama familia zao, hawafuati miongozo na kanuni za utumishi.wa umma.
 
Back
Top Bottom