Wafanyabiashara wa jumla Kariakoo nao kuuzia mali zao barabarani

General Mangi

JF-Expert Member
Dec 21, 2013
15,303
23,058
Hii nimepenyezewa na Moja ya wajumbe wa Umoja wa wafanyabiashara K.Koo kwamba wafanyabiashara wa jumla nao watafunga maduka yao na kuuzia mali zao barabarani kama machinga ili kuepuka kodi za hovyo za TRA, leseni na kodi kubwa zinazotozwa na wenye Fremu.

Wafanyabiashara hawa wakubwa wamekuwa wakilalamika uwepo wa Machinga barabarani ambao hawalipi kodi yoyote wamekuwa changamoto kubwa kupata wateja katika maduka yao.

Sasa mjumbe huyo kasema kwa sasa anarudisha frem na atabaki na stoo tu ya kuhifadhia mali zake, mali za sample ataziweka barabarani na mteja akitaka atapelekwa stoo kuuziwa.

Haiwezekani mimi niuze kitenge kwa 20,000 na machinga huyohuyo anauza kwa bei kama yangu pale barabarani na halipi kodi yoyote.
Tumepeleka malalamiko yetu serikalini lkn hatusikilizwi.

Sasa dawa ya moto ni moto, kama karuhusu machinga, basi na mm nauzia barabarani, alisema mjumbe huyo.

Kwasasa tangu uchaguzi mkuu biashara imekuwa ngumu, hakuna pesa kabisa. Kwa siku ninapata mauzo ya laki mbili huku nikiwa na mali ya milion 300. Kabla ya uchaguzi nilikuwa nauza mpaka milion 25 kwa siku lkn kwa sasa ninapata Mauzo ya laki mbili kwa siku ni sawa na machinga pale barabarani ambaye hana kodi yoyote.

Inasemekana kwamba kumekuwa na bifu zito kati ya wafanyabiashara hawa na Mkulu kutokana na wao kumuunga mkono mgombea wa chadema katika uchaguzi 2015.

Bifu hili ndilo limemlazimu Mkulu kuwakomoa kwa kuwabakiza machinga barabarani.
 
Hii nchi sasa imekuwa ya vilio kila kukicha, huyu mfalme ameingia na mkosi gani? Mpaka sasa hakuna la maana lililofanyika zaidi ya uteuzi na visasi.
 
Sio kkoo tu hata mikoani imekua ngumu.....ukifanya biashara basi serikali nzima inahamia dukani kwako kukusanya kodi mpaka zinajirudia.

Nilichofanya ni kutangaza biashara kwenye mitandao, then samples nimebeba kwenye noah yangu wateja wa mikoani nawatumia........

Maisha yataenda tu
 
Hata ningekuwa mimi ningekaa road pia. Ilaa najaribu tu kuwaza kwa sauti. Hawa wamachinga, hizo bidhaa zao wanazipata kwa akina nani? Sababu kuna wenye maduka wanakuwa wanawapa hawa jamaa bidhaa wauze halaf wanaletewa mauzo badae
 
Hii nimepenyezewa na Moja ya wajumbe wa Umoja wa wafanyabiashara K.Koo kwamba wafanyabiashara wa jumla nao watafunga maduka yao na kuuzia mali zao barabarani kama machinga ili kuepuka kodi za hovyo za TRA, leseni na kodi kubwa zinazotozwa na wenye Fremu.

Wafanyabiashara hawa wakubwa wamekuwa wakilalamika uwepo wa Machinga barabarani ambao hawalipi kodi yoyote wamekuwa changamoto kubwa kupata wateja katika maduka yao.

Sasa mjumbe huyo kasema kwa sasa anarudisha frem na atabaki na stoo tu ya kuhifadhia mali zake, mali za sample ataziweka barabarani na mteja akitaka atapelekwa stoo kuuziwa.

Haiwezekani mimi niuze kitenge kwa 20,000 na machinga huyohuyo anauza kwa bei kama yangu pale barabarani na halipi kodi yoyote.
Tumepeleka malalamiko yetu serikalini lkn hatusikilizwi.

Sasa dawa ya moto ni moto, kama karuhusu machinga, basi na mm nauzia barabarani, alisema mjumbe huyo.

Kwasasa tangu uchaguzi mkuu biashara imekuwa ngumu, hakuna pesa kabisa. Kwa siku ninapata mauzo ya laki mbili huku nikiwa na mali ya milion 300. Kabla ya uchaguzi nilikuwa nauza mpaka milion 25 kwa siku lkn kwa sasa ninapata Mauzo ya laki mbili kwa siku ni sawa na machinga pale barabarani ambaye hana kodi yoyote.

Inasemekana kwamba kumekuwa na bifu zito kati ya wafanyabiashara hawa na Mkulu kutokana na wao kumuunga mkono mgombea wa chadema katika uchaguzi 2015.

Bifu hili ndilo limemlazimu Mkulu kuwakomoa kwa kuwabakiza machinga barabarani.
Mkulu abajikomoa mwenyewe ,kodi ikushuka ataisoma namba na maukali take apeleka porini
 
Nasikia sikuhizi TRA hawabanduki kwa Diamond,,

yaani wakisikia fununu mtu kaingiza tuhela kidogo wanakomalia hapo mpaka wafilisi then wanamove kwa mwingine,
hali ngumu sana
 
Wanachokijua wao toka wamepewa mamlaka ni,
1: Kutumbua
2: Kuzuia mikutano ya kisiasa
3: Kupanda miti Far mpya
4: Kukamatana na kupelekana mahakamani
5: Tanzania ya Viwanda
6: Kupunguza watumishi hewa
7: Kuhamisha sirikali kupeleka dodoma lakini hakuna ofisi za watendaji wake

EMBU JAZIA NYINGINE KAMA UNAKUMBUKA

2020 siyo mbali mtukufu wao kumbuka hii ni 2017
 
Zamani na hata enzi ya Nyerere tulisikia chama kikimshauri Rais anapokosea,sasa siku hizi hao walamba viatu waliobaki wana uthubutu huo?
Kinana unafanya nini kwa nini usijiizulu kuliko kubaki kufanya kazi ya ukarani tuu,au kuna kitu mtukufu anakuogofya?
 
Back
Top Bottom