Wafanyabiashara, ni mara ngapi kwa wiki mnapost content?

Wafanyabiashara, ni mara ngapi kwa wiki mnapost content?

youngkato

JF-Expert Member
Joined
Sep 3, 2014
Posts
3,961
Reaction score
4,131
WAFANYABIASHARA, NI MARA NGAPI KWA WIKI MNAPOST CONTENT?

Kama una biashara na unategemea kupata wateja kupitia mitandao ya kijamii, unatakiwa kuelewa kwamba Content Creation si jambo la kufanya pale unapojisikia tu.

Unahitaji kuwa na consistency.

Usisubiri mpaka uwe na bidhaa mpya, ofa au tangazo ndipo ukumbuke kupost. Tengeneza ratiba ya content ambayo itakusaidia kuendelea kuwasiliana na wateja wako.

Unaweza kupost mara 3 hadi 5 kwa wiki, kulingana na aina ya biashara yako na uwezo wako wa kutengeneza content zenye ubora.

Muhimu si kupost kila siku bila mpango, bali ni kuhakikisha kila content ina kusudi. Iwe ni kuelimisha, kujenga uaminifu, kuonyesha bidhaa au huduma zako, kujibu maswali ya wateja au kuwashawishi wanunue.

Kumbuka, wateja hawawezi kukununua kama hawakukumbuki. Na ni vigumu kukukumbuka kama hauonekani mara kwa mara.

Swali kwa wafanyabiashara: Kwa sasa mnapost content mara ngapi kwa wiki? Mara 1, mara 3, mara 5 au kila siku?
 
Back
Top Bottom