KINAMBUA MDONKOLO
JF-Expert Member
- Apr 18, 2018
- 1,188
- 1,704
kumbe ! Unauza mwenyewe mmiliki wa mzigo au una mpa dalali?Mi navyojua Kile kitendo cha kushusha tani tano za mchele. Halafu bei yako ni affordable kwa mnunuzi wa jumla.
Lazma mchele uishe chapu, tena utagombaniwa.
Ila ngoja waje wajuzi
Sent using Jamii Forums mobile app
Una kabidhiana na hao jamaa au sio?Kuna watu wanajiita madalali hao
wana wameupotezea huu uzi, sijui ni dharau au nini? [emoji17] [emoji22] hata hawachangii ili tujue tuna jikwamuaje.Na mm nasibiria hzo nondo
Nashukuru sanaKuna watu wanaitwa madalali wamejaa masoko yote tz.
Kama mgeni soko husika kuwakwepa ngumu.
Chamsingi ona utaratibu mzuri wa kula nao.
Suala la usafiri magari yako mengi sana bei ni maelewano tu ingawa mafuta yamepanda bei.
Chamsingi fanya survey kwa madalali na wasafirishaji zaidi ya mmoja ili uweze kufanya ulinganifu wa bei na faida utakayoipata.
Kila jema kwako.
#MaendeleoHayanaChama
Nimekupata vipivyo mkubwa kongoleHua kuna madalali lakini inahitaji kuwa makini zaidi ya umakini wenyewe. Hua ni wajanja janja sana. Labda umpate mwenye weledi.
Hua wana tabia ya kung'ang'ania mzigo af kukupa hela inakua story. Wanakupanga kua mteja washampigia sim af wanabaki na mzigo, mtu mwingine akishusha tu mzigo wanakuja kukuoangia bei nyingine ya chini usipoangalia unatoka na hasara kubwa
Kaa ukijua lazma wapate chochote kitu. Sasa hapo ni ujanja wako. Labda ukubaliane kushika hela yako mwenyewe af mwishoni uwape hicho cha juu chao. Cha muhimu usiwe na tamaa. Unaeza kuja unauza kilo moja 2000 ye akapandisha mpka buku 4 kwa mfano na akauza mzigo. Hyo ya juu mpe tu kukwepa matatizo.
Fanya research ujue scarcity iliopo, njoo na mzigo weka bei ambayo itakupa faida na kukufanya usikae sana pale maana kuna risk kibao