Wafanya biashara kandokando ya barabara ubungo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wafanya biashara kandokando ya barabara ubungo

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by bamwaiche, Sep 26, 2012.

 1. b

  bamwaiche Member

  #1
  Sep 26, 2012
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 50
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 15
  Kwa kweli nchi yetu inashangaza na inasikitisha pale inapotumia nguvu nyingi na rasilimali za nchi pasikokuwa na mipango maalum. Nasema hivi kwa sababun na kila mmoja wetu atakuwa shahidi katika hili ama kwa njia ya vyombo vya habari au kwa kushuhudia moja kwa moja. Hii ilikwa ni oparesheni kabambe ya kuwaondoa wafanya biashara wanaoganga njaa kandokando ya barabara ya morogoro alimaarufu stendi ya daladala ubungo. Serikari iliamua kuondoa msongamano huo kwa nguvu nyingi ambapo askari wa kutuliza ghasia walikaa mahali hpo takribani wiki tatu wakizuia kutorudi tena kwa waganga njaa hao.

  Lakini ajabu na kweli kwamba wafanya baishara hao wamerudi eneo hilo hilo la ubungo ila mkusanyiko mkubwa uko barabara ya Sam Mwakangale(Nujoma). Na mgambo wetu hupiga patrol na kujipatia chochote kwa waganga nja hao ili wahalalishe uwepo wao. Hii ndiyo nchi yetu na naona wale askari ndiyo walienda kujianda na milipuko ya Iringa na Morogoro. Kwa nini nchi yetu inakuwa haina mipango thabiti yenye kutekelezeka katika uhalithia wake. Kubwa zaidi ninaloliona ni kwamba kila mipango inayopangwa , na katika wapanagaji hao kila mmoja abuni mbinu ya namna gani atafaidika na mpango huo kwa maslahi yake binafsi na si kwa maslahi ya Taifa.

  Vilevile katika kwaondoa wafanya biashara hawa serikali yao ilikuwa na jukumu la kuwatafutia sehemu mbadala ambayo wageweza kuendeleza biashara zao ikiwa ni pamoja na kuangalia miundombiu ya kufika eneo hilo tenge. KWA MAANA ENEO HILO LINATIKWA liwe mwnzo wa magri yaendayo sehemu mbalimbali ya jiji hili.
   
Loading...