Nimeishi na Mwanamke huu ni mwaka wa tano, japo haikuwa ndoa rasmi. Baada ya taratibu za mahari tu nilimsogeza japo sijafunga naye ndoa ya kidini wala kiserikali. Miaka minne iliyopita, nikiwa mwanafunzi wa chuo UDSM, na yeye nikimwacha nyumbani (Mkoani), niliporudi likizo moja, rafiki zangu walinitonya kuwa yf alikuwa anamegwa na jamaa mmoja ambaye namfahamu alikuwa dereva wa jirani yangu.
Sikumwambia kuhusu maneno niliyoyasikia, ila niliazimia kufanya upelelezi wa kimya kimya, ili nigundue kama kulikuwa na mawasiliana yoyote kati yao, sikufanikiwa. Nikajiaminisha kuwa kama yf alikuwa anafanya hayo, lazima alikuwa smart sana. Baada ya likizo ile nilirejea Dar kuendelea na shule. Likizo nyingine niliporudi, nakumbuka ilikuwa march 12, 2010 nilirudi na unyumba uliendelea kama kawaida. Sikukaa sana, nikarudi chuo, na nilipomaliza chuo mwaka huo, yaani july 2010 nilirudi nyumbani na nikamkuta ni mja mzito, japo muda wote niliokuwa chuo hakuwahi kunieleza kuwa ni mjamzito. Nilifurahi kwa kuwa nilijua sasa nitaitwa baba. Hesabu ziliniambia, miezi tisa ingetimia kuanzia desemba 12, 2010. Mwezi November mwaka huo huo nilikwenda kwenye mahafali Dar, siku tatu tu baada ya kuondoka, kwa mshangao nilipigiwa simu kuwa yf aliugua uchungu wa kujifungua, hiyo ilikuwa November 18,2010.
Kwa hiyo alijifungua mwezi mmoja kabla ya tarehe niliyoitarajia. Hiyo haikunisumbua sana kwa kuwa nilikuwa najua akina mama huwa wanajifungua mimba zikiwa na umri wa miezi saba, japo sijawahi kusikia akina mama wenye mimba zenye umri wa miezi 8 wakijifungua na watoto wakaishi, wangu alijifungua bila tatizo lolote na mtoto akiwa perfect.
Hivi majuzi rafiki yangu kanipa stori ambapo imenitonesha kumbukumbu zangu hizo, aliposema bora aniambie ukweli ambao anaujua siku kuwa yule mtoto nimechomekewa. Kwamba kimsingi, mtoto ni wa yule mtuhumiwa wangu. Na pia kwamba wakati sipo, yf alitoa mimba nyingine ya huyo jamaa. Nikiunganisha dots napata picha kuwa kuna ukweli flani hapo ukizingatia mtiririko wa matukio ulivyokwenda. Na kaniambia mjini pale watu wanaijua sana hii stori na wananionea huruma tu na kunisikitikia. Sasa wanabodi nadhani mnanielewa ninachosema, nishaurini tafadhali, nisije nikafanya vitu vya ajabu kwa kuwa moyo wangu umejaa hasira, ila sasa hivi nipo mbali naye sababu ya majukumu. Kabla sijarudi nishaurini nifanye nini!
ulichunguza hukuambulia kitu.....
Halafu huyo rafiki yako alijuaje kama mkeo alitoa mimba? Yeye ndo daktari? Alimsindikiza kwa daktari?
Ni vyema ukachunguza taratibu pamoja na kuchunguza mwenendo wa mkeo kimya kimya
Pia katika marafiki zako woooooooooooote ni huyo tu mwenye info za mkeo?
Yaani hata nduguzo hawakujua kama mkeo katoa mimba? Hawajui mkeo anatembea na dereva ilhali mtaa mzima wanajua na wanakuhurumia?
Chunguza kaka inawezekana kuna ukweli au hakuna ukweli au rafiki yako ndo mbaya wako
Ingawa kwa ninj mkeo apate mimba asikuarigu?
Kwa nini hata nduguzo wasizungumzie mimba ya mkeo?
nini kirefu cha ''yf''?
Asante BADILI TABIA.
Wewe unajitaftia ulcers. Mimba hutungwa siku isiyojulikana na ndo maana dr wanategemea izaliwe wiki 2 kabla ama baada ya tarehe iliyokisiwa. Hapo tofauti ya siku ingekuwa miezi 3 tungesema. Na acha na stori za mtoto wa miezi 8 haishi, sayansi ilishashinda hayo.
Maneno ya kuambiwa yatakutia wazimu na kukukosesha raha ya maisha. Utasikiliza maneno mangapi? Hebu uishi na mkeo mfurahie mafanikio. Kama kuna lililojificha sali muambie Mungu nionyeshe yaliyofichika. Kama kuna jambo utaliona tu na sikushauri kujigeuza mbwa wa polisi kila siku kumchunguza mkeo.

Mkuu hiyo iko wazi kabisa,huyo rafiki yako anakujali ingawa wengine watamuona muongo,mmbeya.Hapo amua moja piga chini uanze upya au endelea nae huku ukijua siyo mwaminifu.Pole sana,uaminifu katika ndoa siku hizi umekuwa nadra sana.