Wadau hii imekaaje?

Blue Bahari

JF-Expert Member
Aug 21, 2016
1,509
1,632
Wana JF habarini!

Kwa niaba ya Walimu, napenda kujulishwa utaratibu wa malipo uliotumika katika mitihani ya NECTA inayoendelea sasa (form IV & II).

Kuna sintofahamu zimeibuka kutoka baadhi ya halmashauri katika malipo yaliyotolewa kwa wasimamizi wa mitihani hiyo. Ili Mwalimu aweze kuteuliwa kusimamia mitihani hiyo, anatakiwa ahudhurie semina kisha kuapishwa na hakimu na hatimaye kuteuliwa kusimamia mitihani hiyo.

Sasa sintofahamu imeibuka katika bahadhi ya Halmashauri kwa upande wa malipo, na nimezigawa sehemu tatu kama ifuatavyo:

1. MALIPO YA NAULI
Tuchukulie mimi Mwalimu blue bahari na Mwalimu mwenzangu tumetoka shule moja (shule X), tumetumia gari moja kwenda kuhudhuria semina na pia nauli ya aina moja (mfano TZS 8,000/= kwenda tu, hivyo ukijumlisha na Nauli ya kurudia kituoni x itakuwa jumla tshs 16,000/=).

Sasa baada ya kula kiapo, afisa Elimu anatangaza muundo wa malipo ya nauli ambao kimsingi ni wa kustaajabisha. Anatangaza kwamba Mwalimu anayesimamia form IV yeye atarudishiwa kiasi cha TZS 16,000/= wakati yule anayesimamia form II yeye atarudushiwa TZS 8,000/=

Swali
a) Je, kigezo kipi kimetumika katika malipo hayo ya nauli ilihali tumetoka shule moja na tumepanda gari moja?

b) Je, huo ndiyo utaratibu mpya wa serikali (NECTA) katika hili?

2. CHAKULA
Suala la malipo ya chakula kwa wasimazi nalo limezua sintofahamu katika baadhi ya halmashauri. Afisa Elimu anatangaza muundo wa malipo na kusema kwamba "wale wanaosimamia form IV wao watalipwa Pesa ya chakula TZS 10,000/= wakati wale wanaosimamia form II wao watalipwa TZS 5,000/=". Na wakati huo huo yule anayesimamia kidato cha nne na cha pili wote wanasimamia shule moja na mazingira ni sawa.

Swali
a):Je, kigezo kipi kimetumika katika malipo hayo ya chakula ilihali anayesimamia form IV na yule form II wote wako shule moja?

b) Je, huo ndiyo utaratibu mpya wa serikali (NECTA) katika hili?

c. Je, hiyo TZS 10,000/= au 5,000/= inatosha kwa siku zote za mitihani kwa chakula cha Mwalimu.

3. MALIPO YA USIMMIZI WA MITIHANI
Hili nalo limezua mkanganyiko mkubwa katika baadhi ya halmashauri (hususani Bunda vijijini), ambapo walimu wamelipwa kulinganana na mikondo uliyosimamia.

Mfano, Mimi Mwalimu Blue bahari nimepangwa mkondo " C" katika shule X, ambayo ina vyumba vitatu vya mitihani wa kidato cha nne na kuna walimu wengine wanaosimamia mikondo "A na B". Mimi wa mkondo C sitalipwa pesa ya usimamizi wa mitihani ile ya practical (kwa kuwa wanakuwa wachache ukiondoa biology), hivyo anayesimamia mikondo A ndiyo atakayelipwa pesa hizo za usimamizi practical za chemistry na physics. Na ndiyo maana kuna bahadhi ya wasimamizi wamelipwa pesa ya siku tano, wengine sita wengine saba n.k

Swali
a. Je, ni utaratibu mpya wa Serikali (NECTA) halmshauri zote?

Nimeleta kwenu uzi huu ili kuwekana sawa kwa kuwa ni matumaini yangu kwamba kuna wadau wengi wa elimu wanaopita jukwaani humu katika kupashana habari. Vile vile bila kusahahu pia watumishi wa serikali nao wanapitia humu.
 
Back
Top Bottom