Habari za asubuhi wana JF,
Leo nimekutana na kituko cha mwaka katika hospitali yetu ya mkoa wa Mwanza Sekoutoure. Nilienda kumjulia hali jirani yangu amelazwa. Pembeni yake kulikuwa na bibi ambaye alikuwa anatapatapa katika kumalizia kukata roho.
Yule bibi akawa ana lalama kwa lugha ya huku kwetu ya kisukuma akisema MAAYOO MAAYOO yaani MAAMAA MAAMAA, hapo wodini kulikuwa na mabinti wawili ambao anao walikuja kwa minajili ya kumsalimia mgonjwa wao.
Wale mabinti wakawa wanacheka wanamuangalia yule bibi anayetapatapa kukata roho, nikawaauliza mbona mnamcheka bibi wa watu? wakanijibu tena kwa kujiamini kabisa: "INACHEKESHA YAANI HAKA KABIBI NAKO ETI KANAVYOKATA ROHO KANAMTAJA MAMA YAKE"
Baada ya muda mfupi bibi aliaga dunia.
Sikuwasemesha tena hao wadada, zaidi ya kuwashirikisha wana JF wenzangu kuwa duniani kuna vituko!