Wadada Ndivyo Sivyo

supercharger GT

JF-Expert Member
Sep 25, 2016
1,017
1,965
Hii imekaaje wakuu? Kuna wanawake wa aina flani kwa kweli nashangaa.

Hapa kazini kuna jamaa fulani yupo kitengo tofauti na mimi, ila tunasalimiana! Jamaa mtanashati na mpambanaji kisawa sawa. Kupitia story za jamaa yake wa kitengo hicho,

Nasikiaga alipitia maisha magumu sana kuanzia kusoma, maisha ya kutafuta kazi e.t.c, Sasa wakati anatafuta kazi maisha ndo yakiwa magumu haswaa ndo alikutana na mrembo fulani wakaivana.

Huyu mrembo alikuwa mvumilivu ajabu, na huyu mrembo kwao sio kwamba wana maisha mazuri La Hasha ni kawaida tu ila hawana njaa na hakufanikiwa kufika chuo so yupo tu nyumbani.

Miaka imeenda kama minne hivi jamaa hajapata kazi na mwanamke yupo tu, sometimes anaenda gheto kwa mshikaji na buku buku hizi au buku mbili na mchele kaiba home kwao wanapika maisha yanaendelea.

Cha ajabu jamaa kaja kapata kazi, maisha yakanyooka na nyota ikamuendea vizuri kipindi kile mikopo nje nje kachukua mkopo kajenga kanyumba kadogo fresh na kigari cha kutembelea, hapo ndo maajabu yakatokea, si mwanamke akamuacha bila sababu ya maana! Jamaa ashaweka yule ndo mke wake wa baadaye kwa waliyopitia ila mwanamke kakataa kata kata!

Sababu anazosema ni eti anaona havutiwi tena na yeye, na anaona kama hamjali kama zamani wanawake wa namna hii sijaelewa huwa wanakuwa wanakuhurumia ukiwa na matatizo au ni vipi? Au ni wale wanaletwa na Mungu ili usijiue kwa matatizo ya dunia???

Kuna anayeweza fafanua hii Scenario humu???
 
Mhh hii mpya ila mi navoona inawezekana mdada hajiamini(insecured) kahofia ushindani ambao ungeanza maana maisha yameanza kuwa mazuri na wanawake wengine pia wataanza "kumuona" tofauti na mwanzo jamaa hana hela.

Ila pia yaweza kuwa mengine
 
Mhh hii mpya ila mi navoona inawezekana mdada hajiamini(insecured) kahofia ushindani ambao ungeanza maana maisha yameanza kuwa mazuri na wanawake wengine pia wataanza "kumuona" tofauti na mwanzo jamaa hana hela.

Ila pia yaweza kuwa mengine
Haijawahi kutokea na ni moja kati ya thread zenye kumzungumzia mwanamke tofauti na ilivyozoeleka
 
Utafiti gani wa miaka kila siku tunatishiwa kufukuzwa maabaraa aah wabaki wenyewe na wewe pia mtafute wengine.

Posho yenyewe mbinde
Ni jana tu tumetoka kwenye Valentine, wewe naye unaanza kutuchosha wakati tunafungua maboksi ya zawadi.

Kuna utafiti juu ya tabia za wanawake anaufanya Asprin chini ya ushirika wa Bonny, Numbisa na emmyta; wanaweza kukueleza kwa kifupi tu wapi wamefikia.

Mimi kama mimi hapo umeniacha njia panda.
 
Mkuu stori kadri inavyotoka kwa mtu mmoja kwenda mwingine ndivyo inavyopeteza uhalisia sababu kila mtu ataongezea au kupunguza yake. Kwa maelezo yako ni kwamba hizo habari hazijatoka moja kwa moja kwa mhusika.

Lakini hayo maelezo pia yametoka upande mmoja (one sided). Sidhani kama kuna mwanamke anayeweza kudumu na mwanamme katika kipindi kigumu halafu aje kumuacha baada ya mafanikio, tena kwa sababu isiyo na msingi kama hiyo. Mi nadhani kutakua na sababu nyingine yenye uzito ambayo jamaa hayuko teyari kuisema.
 
Wewe huyo jamaa humjui kama huyo demu anyo mjua

Atakua amechange kweli kwa kupata vipesa mboga na ndio sababu ya kukataliwa na dem huyo,wanawake sio wajing kiasi hicho akukubali wakati wa dhiki na akukatae wakati wa raha

Huyo Jamaa lazima ajicheki tabia yake imebadilikia wapi na abadilishe mapungufu yake
 
Ndoa muamini kwamba si kila mwanamke yuko after money
Jiulize huyu mambo yamenyooka ndo anakaa pembeni..

Inawezekana jamaa baada yakupata pesa alionyesha vijitabia ambavyo binti aliona hataviweza vikikomaa

Akaona isiwe tabu niwapishe wengine. ..
 
Hao wana mpango wa kuvunja rekodi watatoa kitabu kikubwa sijui kama shati la nani.
Ila ndio litakuwa limejaa uongo mtupu.

Tutarudi kwenye ule usemi usemao "ukubwa wa pua sio wingi wa makamasi"

Hivyo tusubiri tuone
 
Ndoa muamini kwamba si kila mwanamke yuko after money
Jiulize huyu mambo yamenyooka ndo anakaa pembeni..

Inawezekana jamaa baada yakupata pesa alionyesha vijitabia ambavyo binti aliona hataviweza vikikomaa

Akaona isiwe tabu niwapishe wengine. ..
Hiyo Avatar ni yako ?
 
Sitaki kuamini. Yaani mwanamke kwenye raha ndio hamtaki mwanaume.

Ni katika dunia hii tuliyonayo ama nyingine.

Lazima kuna kitu nyuma ya pazia
Mkuu ndo maana hapo kwenye thread nmeeleza kabisa kuwa hata mm nashangaa, na sijawahi kukutana kabisa na story kama hii!!!!!
 
Sitaki kuamini. Yaani mwanamke kwenye raha ndio hamtaki mwanaume.

Ni katika dunia hii tuliyonayo ama nyingine.

Lazima kuna kitu nyuma ya pazia
Mkuu ndo maana hapo kwenye thread nmeeleza kabisa kuwa hata mm nashangaa, na sijawahi kukutana kabisa na story kama hii!!!!!
 
Back
Top Bottom