Hivi mpaka karne hii ya 21 bado watu wanahoji uwezo wa wanawake? Nadhani kunatatizo la kukaa madarasani bila kuelimika. Wanawake wasichoweza kufanya vizuri ni ukuli wa kubeba magunia kupandisha kwenye basi za zamani. Kama kazi inahitaji kutumia ubongo wanaweza sana.
Hivi matokeo ya mitihani kwa Dr. Ndalichako hamyasikii au mmegoma? Mama Ndalichako mwenyewe mwaka huu ameweza jambo ambalo mabosi wanaume liliwashinda la kuzuia mitihani isivuje sembuse biashara ya kununua na kuuza. Wanaweza na wanamitaji na wanaaadabu ya hela tofauti ya wenzangu mimi. Kama unabisha nenda kwenye mabenk wanakochukua mikopo ukaone kuna nini? Ni wakopaji wazuri tofauti na wenzangu na mimi.