Wadada Inawahusu hii


Nani alikuambia ni hobby, unajidanganya danganya sana ndo nyie hamchelewikuja huku mkilia oooh! ndugu wa mchumba wangu hawanitaki wakati unajua faimilia za kiafrika n extended labda utaolewa ulaya......
 

Waswahili wanasema dua la kuku......sasa sikiliza, je nikiwa sijui kupika siwezi kuwa mke mwema au mama mwenye familia bora. Nani aliysema mwanamke lake jiko tu, kama ni hivyo angetafuta mwanamke chef wa kuoa, mimi kwangu kupika sio prerequisite katika swala la ndoa na wala sijaona ndoa zilizovunjika kwasababu maza houz hajui kupika.

On serious note binti2013 na hizi standardisation za sijui mtoto wa kike akiwa 15yrs lazima ajue kupika...ooh please doens't apply to everyone. Kwa umri huo kuna vitu binti anapaswa kuvijua zaidi kabla ya kujua kupika... kama nilivyosema mwanzo, usafi wake wa mwili na mazingira anayoishi..... Hoja yangu ni umri huo wa 15 hata ajue kila kitu haendi kuolewa kesho, binti ajifunze kupika when she feels ready kwani kulea kila mtu anaformula yake.

Nimegundua kitu kimoja hii mambo ya kufosi mtu pika au mafunzo ya nguvu saa nyingine si mazuri, labda mama ataona fahari mtoto wake ana umri 15 anajua kusonga ugali wa watu 20 lakini hakuna kitu kizuri kujifunza kama pale unapokuwa tayari kujifunza na kwa mapendekezo yako mwenyewe maana utakuwa unapika with passion.

Ushawahi kusikia wale wanaopika kwa ajili watu wasife....maana no interest at all...ni mvurugano gani lakini huna hila, sababu mojawapo ni inaweza kuwa ameanza kupika mdogo sana...

cc Tamatheo, Ngalikihinja
 




hapo chacha!
 
kwa mwanamke hasa aliye kwenye ndoa kujua kupika ni muhimu ( ustadi katika mapishi unatofautiana kulingana na mazingira tuliyo kulia, na interest pia) lakini hili si jambo la kupuuzia, binafsi nimeshuhudia ndoa yenye mgogoro kwa sababu mke alikuwa hawezi kuandaa chakula
 
CC
MadameX
Nivea
 


Ukute wanaopinga imewatachi .
 

Pole kwa kutokujua ila ukweli utabaki palepale kwamba mtoto lazima ajue kupika na sio kwa kufundishwa ila kwa kuona kwa mzazi kama ilivyo kwa usafi na mambo mengine. Hili la kuamua mtoto ndio ninaposema malezi mabaya ya mtoto kumlea mzazi na sio mzazi kulea. Mpe mwanao tunu njema za malezi ili aweke kumbukumbu ya maisha yake yote.
 

Mwanamke kujua kupika ni kitu kikubwa sana katika familia, nakubali kuwa tuna shughuli mbalimbali zinazotufanya tusiweze kupika kila siku, ila walau mara moja kwa wiki siyo mbaya hasa watoto wakajua kuwa mama leo katupikia chakula.

Ukipika mama watoto wanafurahia sana na kushukuru sana kwa chakula kizuri na kitamu. Tusikwepe majukumu kwasababu zisizo na lazima.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…