Wadada Inawahusu hii

Binti1

JF-Expert Member
Joined
Jul 8, 2013
Posts
668
Reaction score
1,766
Ndio upo busy sana. Kuanzia form one umesoma boarding hadi degree na baada ya hapo umepata kazi unatoka nyumbani sa12 unarudi sa 2 usiku. Lakini hii sio sababu ya kukufanya usijue kupika. Haipendezi msichana wa zaidi ya miaka 15 akiwa hajui kupika chakula kizuri watu wakala wakafurahi. Hauolewi ili uende kupika lakini kumbuka kila siku inawapasa kula. Kila msichana lazima ahakikishe anajifunza kupika, hakuna anayezaliwa anajua kupika ila ni kujifunza na kupika mara kwa mara.

Usimtegemee tu dada wa kazi ndiye akupikie, hata akipika vibaya hutakuwa na ujasiri wa kumkosoa. Watoto na mume hujisikia vizuri wakipikiwa chakula mama/mke.

Kwa wale walioolewa hakikisha kila wiki kuna siku ambazo unapika wewe mwenyewe kwa ajili ya familia yako. Sio kila siku kila wiki kila mwezi ni dada wa kazi tu ndiye anayepika.

Yani ufanye bidii uwe unajua kupika zaidi ya dada uliyenaye hadi ifike mahali ukipika chakula wote wajue mama leo aliingia jikoni na wakati mwingine wakuombe uwapikie kitu fulani maana wanajua wewe ndiwe mtaalamu.
 
Watakuwa wanakula hotelini, wanaogopa kuungua vidole na mikono .....................!:tape:
 
kupika sio common need kwa binadamu kama wewe hujui wengine wanajua waajiri wakupikie ,ujue kila kitu isaidie nini wanaosomea chefs wafanye nini?kha
 
Nivea mama usipotoshe watu itakua umesema hivyo kuchangamsha genge !!!!
Kama ulichosema ni kweli nipe fact ya mwanamke aliyeeolewa na hajui kupika?Hata kama utaajiri mpishi mwanamke unatakiwa ujue kupika hiyo ni moja ya sifa kuu za mwanamke.....sio umeolewa unaingia jikoni kwako hujui chumvi inakaa upande gani hujui mwiko uko wapi....sana sana utamuaibisha mama ako tu kwa usista duu usio na tija!
Mwanamke na jiko mwanamke mapishi......Kuna tofauti na raha mumeo na watoto wanayoisikia wanapokula chakula ulichopika mama wa nyumba.
 
binti2013, nasema yategemea malezi, mila na desturi. Unaweza ishi bila kupika ......na nani aliyesema mwanamke ni LAZIMA ajue kupika ndio awe mama wa nyumba. KUPIKA au kuwa mpishi hodari na added advantage ya mwanamke lazima sio kigezo.

Nafikiri ungesisitizia mwanamke USAFI...unaweza ukawa mpishi mzuri usafi ukakushinda bibi, all your effort in drain maana hata chakula chako hygiene itakuwa problem. Na pia hiyo ni sifa ambayo inakipaumbele zaidi ya upishi.

Mwanamke tabia, ujue vipi kulea family yako na kufanya family bora.......
 
kupika sio common need kwa binadamu kama wewe hujui wengine wanajua waajiri wakupikie ,ujue kila kitu isaidie nini wanaosomea chefs wafanye nini?kha
Nivea.....labda unaongelea utamaduni wa kizungu.Kwa waafrika ni muhimu mwanamke akajua kupika.Tena kupika vizuri.Ni aibu hata kwa wakwe zako kama hata kupika hujui infact hata huyo mume si ataanza kulalamika?
 
kupika sio common need kwa binadamu kama wewe hujui wengine wanajua waajiri wakupikie ,ujue kila kitu isaidie nini wanaosomea chefs wafanye nini?kha
Ngoja chefs waje wakubebee mwanandoa wako..... kama hoja ndo hiyo, kunasiku utauliza..''machangudoa wanafanya nini..??? Hivi unadhani hakuna unachomfanyia mwenzio hawezi kukipata nje....?? Kama ni watoto anaweza akazaa nje, kama ni kula anaweza akala hadi kwa mama ntilie, kama ni kufua dry cleaner za kumwaga, kama ni maneno matamu matamu anaweza akayapata nyumba ndogo mwanzo mwisho....

Msije mkadhani anachotakiwa kukipata kwako ni kile kisichopatikana nje.... VYOTE VINAPATIKANA, SASA WEWE WA NINI KAMA UNADAI CHEFS WAPO..??
 
Nivea.....labda unaongelea utamaduni wa kizungu.Kwa waafrika ni muhimu mwanamke akajua kupika.Tena kupika vizuri.Ni aibu hata kwa wakwe zako kama hata kupika hujui infact hata huyo mume si ataanza kulalamika?
Kuna watu wako very theoretical when it comes to ndoa.... Wao ukiwagusia hayo aliyoyasema binti2013, utawasikia... MFUMO DUME....... Na usishangae mtu kama Nivea, kala vyakula vya kupika mama yake mzazi mwanzo mwisho, lakini yeye anataka aje awalishe wanawe na mumea misosi ya house girl in the name of haki sawa.

Ningeelewa sana kama angalau
Nivea angesema mpike wote, yaani baba, mama na beki tatu.
 

waambie hao!! hapa umemaliza kila kitu!!
 
MadameX nakuelewa sana but tuongelee desturi na mila zetu za kiafrika coz thats what we are....Najua usafi muhimu,tabia njema na heshima muhimu,mambo kibao muhimu but thread inaongelea issue ya MWANAMKE KUJUA KUPIKA.....kwa upeo wako labda na malezi wewe unaweza kuona sio muhimu but kwa binti aliye lelewa na mama anaelewa maisha ya ndoa hawezi kua proud kuona binti yake ameolewa hajui kupika.Mi naona Chef/wapishi wanakuja baadae sana kama wasaidizi waziada pale mwanamke unapozidiwa na majukumu bt Mwanamke kupika muhimu!
 
Nivea.....labda unaongelea utamaduni wa kizungu.Kwa waafrika ni muhimu mwanamke akajua kupika.Tena kupika vizuri.Ni aibu hata kwa wakwe zako kama hata kupika hujui infact hata huyo mume si ataanza kulalamika?
Wakwe kitu gani bhana?! kwani unatakiwa kujua kupika kwa faida ya wakwe? ungesema ni kwa faida ya mtu mwenyewe ningekuelewa. tusilazimishe vitu kwa sababu wengine watatuonaje, ndo mana hatuendelei manake tunabaki kufanya vitu ambavyo si lazma sana ili tu watu wasitujaji vibaya. By the way, kupika ni hobby.
 

kama vyote hivyo anapata huko nje, sasa anaoa ili iweje? si aendelee kupata huko nje maisha yaendelee...?!
 
Ndo maana makaumuni yanaajiri watu wa PR mamaa(hao extras nao ni muhimu,unless kama hujaolewa bado).....wewe unafikiri uzuri na usafi tu ndo mambo ya msingi?Na unataka kutuaminisha kwamba ukiolewa kama hujui kupika ni poa tu?Believe me kama hujui kumpika mumeo na watoto vizuri hilo ni tatizo tena kubwa tu(labda kama umeolewa na mzungu)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…