Wadada beware of destiny

Wadada beware of destiny

Samcezar

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
13,093
Reaction score
22,806
Naandika hii post kwa hisia nzito kwa watoto wa kike especially ambao wameshapevuka na wamevuka umri wa miaka 18 kama haujafika umri nenda kabadili diapers kwa mama .......

Okay ni hivi......destiny kwa kiswahili ni hatima au mwishoni. Akina dada nawapenda sana hadi kuwaambia maneno haya mazito........dada zangu......mdada unapokuwa unafwatwa na wanaume wengi haimaanishi wote ni wako.......bali unatamaniwa.......kuna mdada hapa mtaanaani alikuwa ni mkali balaa siku za nyuma ila sasa stress za upweke zinamharibu muonekano anakuwa kama mzee na hata akili yake now sidhani kama ipo sawa ingawa ana elimu kiwango cha degree......
Huyu dada alikuwa strict mbaya.....sisemi alikuwa anaringa. Miaka ya nyuma kila aliyekuwa anamtaka alichezea cha mbavu. Alikomaa na shule tu.....akirejea likizo ni ndani muda wote. Sidhani kama huyu dada alikuwa na mtu.....
Miaka ikapita watu tukawa hatumuone tena kitaa......wajanja tukajua tu kuwa goma limebebwa mazima na jinsi alivyokuwa mkali.
Sasa juzi kati nimetimba kitaa kijiweni namuona anapita kamshika mtoto wa kama miaka 9 hivi. Wadau wakanitonya kuwa wanamuona mbona longtime alirudisha majeshi home kwao kwa bi mkubwa......life la ndoa limezingua......akarudi kitaa akazuga miezi michache ghafla akaanza kurudishwa na audi ya mume wa mtu.........mwenye mume aliwafumania huko akagawa dozi kwa bi dada ongezea na mikasa miwili mitatu ya kutoka na njemba tofauti zilizompotezea muda kisha zikamwacha solemba........
Sasa bi dada yupo kitaa tu.......hayupo sawa.......si tena yule ninayemjua uzuri unafifia........mwanzo alikuwa mkimya na haonekani kitaa ila now anaongea huyo kama chiriku.....yupo yupo tuh busy for nothing church kwa sana.......
Nikashika tama nikasema mmmmmmmmmmhmn kweli binadamu tunapanga ila yupo anayeamua hiyo mipango iwe ama isiwe.........usifanye mchezo na destiny.
 
Natamani kujua alichokosea huyo dada ni nini maana sijaona tatizo lake hapo....katika wale waliomtokea akamchagua mmoja ila bahati mbaya ikabuma...yeye angejuaje? Destiny ipo tu...there's nothing u can do about it
 
Hata mimi hadi nimerudia kusoma tena kama sijaelewa hivi, if its a mater of destiny then tatizo letu ni nini?? Au tufanye nini sasa?
 
Ukimpenda mtu bwana..... ukimtaka mtu mwambie ukweli sio kumpakazia.

Naimba tu.
 
Hata mimi hadi nimerudia kusoma tena kama sijaelewa hivi, if its a mater of destiny then tatizo letu ni nini?? Au tufanye nini sasa?

hapo angerukaruka na mabwana bado angesemwa
 
Hata mimi hadi nimerudia kusoma tena kama sijaelewa hivi, if its a mater of destiny then tatizo letu ni nini?? Au tufanye nini sasa?

Mwandishi anamaanisha wadada muwe mnachangamana na watu tofauti tofauti wake kwa waume mngali bado wasichana ili muzijue mbivu na mbichi na akili yenu ipanuke zaidi kijamii, ili mkiyapata ya jamii ( ikiwemo kuolewa na kuachika) muweze ku adjust vyema na kuendelea na life kama kawaida. Too much Strictness kama huyu dada, inakuweka mbali na reality ya maisha!
Nimemuelewa Mwandishi kihivyo!
 
ukichagua nazi sana lazima uangukie koroma.... tatizo siyo uzuri tatizo ni choice ... wanawake bwana atakuta anapendwa lakini utakuta yeye anapenda asipopendeka na kukimbizana nako...... pale unapoona unapendwa unajisikia amani, unajisikia kuwa huru na huyo mwenzio.. na unaona utaweza kuwa honesty kwake na ukahisi some how yupo honest kwako just be with that person...... japo mimi naangalia yote hayo na pesa
 
Natamani kujua alichokosea huyo dada ni nini maana sijaona tatizo lake hapo....katika wale waliomtokea akamchagua mmoja ila bahati mbaya ikabuma...yeye angejuaje? Destiny ipo tu...there's nothing u can do about it
Alikosea kugawa utamu ovyo. tulizeni vipochi manyoya hivyo hadi muolewe. Inawezekana kabisa na wala hakuna ugumu wowote.
 
Back
Top Bottom