Mkuu, nimechelewa sana kuiona hii post yako. Ndio naiona leo. Ndio mkuu mimi ni mtaalamu sana wa Project Planning na Business proporsal. Nilijikita sana kwenye agribusiness sector. Saiv nipo kwenye shughuli nyingine na ninaendelea na miradi yangu midogo midogo
Soko la sisal lipo na ni la uhakika. Vipo viwanda na makampuni yananua sana sisal fibres. Kuna kiwanda kinaitwa TANCORD 1998 LTD kinamilikiwa na Katani ltd pale tanga kinanunua sana sisal fibres. Kuna kampuni za Moh bila shaka nao wananunua sisal fibres. Soko kubwa zaidi ambalo hata haya makampuni yanauza ni United Kingdom. UK ndio anasambaza maeneo mengine duniani. Price per ton inategemea na grade unayozalisha. Grade inayozalishwa zaidi Tanzania ni UG na SSUG. Price inaenda 2M per ton mkuu ila huwa ina fluctuate kutegemea na global production