Wachina wamiminika nchini, kulikoni? Immigration wanatoa vibali kiholela?

anti-fisadi

JF-Expert Member
Nov 20, 2010
368
31
attachment.php


takribani wiki sasa imekuwa ikionekana ndege zikishuka na wachina lukuki na airport kujaa kama vile tupo beijing!!
kulikoni jamani?? ndege aina ya boeng imejaa wachina zaidi ya mia mbili kama wanavoonekana pichani hapo ni vipi? je wamekuja kwa visa ipi? utalii? kazi?

Hivi sasa sie kupata vibali vya kiabiashara kwenda china imekuwa ngumu sana, kwa taratibu walizoweka nchini mwao; wanataka waje wajenge viwanda kurasini kule ili sie tusiende kwao. Sasa ndio hivi wanakuja kuchukua ajira zetu?? vijana wa kitanzania waendelee kukaa vijiweni?

kwanini na sie tusiweke mazingira magumu wao kuingia nchini kufanya kazi ama biashara? au nani anafaidika nao??

nawasilisha
 

Attachments

  • IMG-20130108-WA000.jpg
    IMG-20130108-WA000.jpg
    41 KB · Views: 905
Nchi imeuzwa kwa wachina! Bodaboda,simu,tv,subwoofers.......Yaani nikikaa ndani mwangu, kila kitu china! yaani nilifikiri labda ' kufuli ' langu sio china! Nimeangalia jana nalo limepigwa chata CHINA! Moyo tu na akili yangu ndio sio ya kichina. Sasa hawa jamaa wanaanza kuchukua nchi polepole
 
Sasa huoni sisi tutakuwa na hali nzuri kama watajenge viwanda huku ama wewe unafurahia kwenda kwao?
 
Yesu Tanzania kwa kadri siku na miaka inasogea inakuwa shamba la bibi kutokana na udhaifu mwingi. Kwa hakika katika vile viwanda vya wachina kwenye maeneo ya makazi ni wameajiriwa wao hadi ulinzi!! sasa kwa nini Boeng isijaze vibarua toka china!! Nchi dhaifu itakuwa dhaifu hata kwa nzi!!
 
Yesu Tanzania kwa kadri siku na miaka inasogea inakuwa shamba la bibi kutokana na udhaifu mwingi. Kwa hakika katika vile viwanda vya wachina kwenye maeneo ya makazi ni wameajiriwa wao hadi ulinzi!! sasa kwa nini Boeng isijaze vibarua toka china!! Nchi dhaifu itakuwa dhaifu hata kwa nzi!!
Mkuu Zogwale swala la Yesu ni typing error au kuna ujumbe ulitaka kuutuma,maana naona kama inaninginia?
 
Last edited by a moderator:
US kila siku wanaingia maelfu ya watu toka nchi mbalimbali na hatujaona wakilalamika kua ajira zao zinaibiwa...what mattars ni vibali vya kuishi nchini ndo muhimu same as ukienda UK hawajali chamsingi kibali chako kikiisha muda wake wanakufatilia uondoke..swala la wachina kuja nchini kwa wingi kwanza lina faida zake nyingi kuliko hasara unazosema za ajira.....ACHA UOGA CHANGAMKA WAKATI NI HUU
 
Bora wao wamakuja kufanya biashara unajua watanzania wanafanyanini china na hongkong wengi wao ?! I wish sikumoja nikuchukue ukajionee maajabu ya nduguzako kule..?

Kwa taarifa yako nowadays watanzania wa atumie boda la hongkong kuingia china coz hongkong viza unapewa unapofika airport...na china wanakila haki yakuwafanyia ugumu jinsi watanzania wanavyotia aibu wengi wao wezi na makahaba
 
US kila siku wanaingia maelfu ya watu toka nchi mbalimbali na hatujaona wakilalamika kua ajira zao zinaibiwa...what mattars ni vibali vya kuishi nchini ndo muhimu same as ukienda UK hawajali chamsingi kibali chako kikiisha muda wake wanakufatilia uondoke..swala la wachina kuja nchini kwa wingi kwanza lina faida zake nyingi kuliko hasara unazosema za ajira.....ACHA UOGA CHANGAMKA WAKATI NI HUU

dah ... unalinganisha taifa lisilo na mwenye asili-USA na taifa la Tanzania?

anyways thank you for this useless post
 
Mbona nyinyi muko Watz wengi kule china kama ufukwe wa mchanga wa pwani, kwa ufupi tafutni kazi ya kufanya kama hamuna kazi musiangalie watu huu ni umbeya
 
Unakumbuka mkataba alioingia Mr Dhaifu na Wachina ili wasimnyonge mwanaye aliyekamatwa na madawa ya kulevya huko China?
Haya ni matokeo ya mkataba na makubaliano baina ya CHINA na TZ kupitia kwa Dhaifu.

UMEONA EEEEEEEEEEEH, NILIKUA NAJIULIZA LILE DILI LA RIZMOKO KWA MZEE HUJINTAO LILIKUWA KANYBOYA NINI???????
KUMBE JAPO NI SHAM AGREEMENT LAKINI UNATEKELEZEKA?????????? DUh
 
Mimi siwaelewi ndugu zanguni, ninachofahamu sio wachina tu hata wahindi pia na wengineo. Uamuzi wa kuwakubali wageni au kutowakubali wageni uko mikononi mwa watanzania wenyewe.

Ikiwa wageni watakuja hapa kwa nia nzuri za kushirikiana kibiashara nadhani ni jambo jema lakini kama wageni wanakuja hapa kwa nia ya kulihujumu taifa letu ni jukumu letu wananchi kuwasusia bidhaa zao na kutoshirikana nao, mfano mzuri nenda ukaone katika mikoa ya Kilimanjaro na Arusha.

Kama mgeni akifika katika mikoa hiyo niliyoitaja ni lazima wajue nia na madhumuni ya kuja kwake, ikiwa amekuja kuchuma na kuhamishaa rasilimali zao wanamsusia biashara zake na si muda ataamua kufungasha virago na kusepa.
 
Acheni xenophobia.

Kama mna issue specific, wameingia bila vibali, au wameingia kufanya kazi ambazo Watanzania wanaweza kuzifanya, wekeni hapa.

Else mnaonekana xenophobes tu. Hamna tofauti na Warusi skinheads wasiotaka watu weusi waende kusoma kwao.

China sasa hivi uchumi wao unakua kwa kasi sana na inatengeneza matajiri wengi sana, mwaka jana Uingereza wamesema wamepata a record number of Chinese tourists, who helped boost the economy.

Sasa mnaweza kufikiri mna uzalendo kumbe mnakataa watalii. Mtalii si lazima awe mzungu mjue.
 
Tatizo elimu ya Tanzania ipo kwenye vyeti zaidi, ujuzi hafifu.Acha wachina wapige kazi kwani wametawala kila sector.
 
gas,na hivi ndo watajenga bomba basi hata mama lishe watakua wachina,hii ndo Tanzania
 
Back
Top Bottom