Wachina wamevunja sheria gani

Wachina wamevunja sheria gani

Rihana

JF-Expert Member
Joined
Apr 26, 2013
Posts
498
Reaction score
250
Kumekuwa na matamko mbali mbali yakikemea raia kutoka china wasijihusishe na kufanya biashara ndogo ndogo, hivi kufanya biashara ndogongodo ukiwa raia wa nche ni kosa kwa mujibu wa sheria gani. Ninavyofahamu mimi Fair competition Act ya 2003 inazuia uingizaji wa bidhaa zisizofikia kiwango lakini sheria hii haielezi kwamba kuwa raia wa nje haruhusiwi kufanya biashara nchini. Kuna kisingizio kingine kwamba wachina wanaingia nchini kwa kisingizio cha 'investors' only to find them hawking lakini kwa mujibu wa TIC ACT investors ni wale wenye mtaji kuanzia dola 100,000. Je wachina kuja nchini kufanya biashara wamevunja sheria gani?
 
Umetumwa wewe...! Acha kuwapa ma------ wachina. Kwa hiyo wamekupa shi ngapi ili uandike hivi.
 
No sijatumwa I am just curious( there are so many discrepancies in our legal system)
 
Sheria iko wazi kabisa,raia wa nje anatakiwa aje nchini kuwekeza na si kufanya uchuuzi,ina maana akija hapa anakuja na mtaji na kuanzisha ajira mpya si kufanya kazi ambazo wazawa wanazifanya.........

Sent from my BlackBerry 9900 using JamiiForums
 
To begin with, you could then discuss on those statutes' discrepancies rather than advocating the chinese vandalism in our country.
 
Sheria ipi can you be specific? Fair competition Act? Investment Act of 1997? your statement is so vogue!
 
To begin with, you could then discuss on those statutes' discrepancies rather than advocating the chinese vandalism in our country.

"chinese vandalism in our country" this is too sweeping statement, isn't it?
 
Kumekuwa na matamko mbali mbali yakikemea raia kutoka china wasijihusishe na kufanya biashara ndogo ndogo, hivi kufanya biashara ndogongodo ukiwa raia wa nche ni kosa kwa mujibu wa sheria gani. Ninavyofahamu mimi Fair competition Act ya 2003 inazuia uingizaji wa bidhaa zisizofikia kiwango lakini sheria hii haielezi kwamba kuwa raia wa nje haruhusiwi kufanya biashara nchini. Kuna kisingizio kingine kwamba wachina wanaingia nchini kwa kisingizio cha 'investors' only to find them hawking lakini kwa mujibu wa TIC ACT investors ni wale wenye mtaji kuanzia dola 100,000. Je wachina kuja nchini kufanya biashara wamevunja sheria gani?
Hili swala hata mi mi nimewahi kulifikiria sana na nimeona tabia yetu ya uvivu ndio inatufanya tuwapakazie hawa wachina.

Unaweza ukawa unaishi mazingira fulani lakini ukawa hauna ubunifu wa kuyatumia yalae mazingira ili kujikwamua kimaisha ,lakini akaja mgeni na kuyatumia mazingira yale yale kwa mbinu mbadala na kuweza kutengeneza uchumi kabambe.

Watanzania tumebaki kuwa walalamishi kila kukicha kazi hatufanyi na kila mmoja anawaza kuwa diwani au mbunge hata maprofesa wa chuo kiuu?nani atunge vitabu?nani akosoe pale wanasiasa wanapokosea?unaenda bungeni unaudhalilisha uprofesa pale ambapo jamii inategemea makubwa kutokana na status yako lakini unashindwa? Eti kila mtu akijua tuu kuongea anajiita mwana harakati ya wapi hii?

Inatakiwa tukae na hawa wachina tena wajasiriamali kwani ndio tuko nao mitaani sio wale wawekezaji,tujifunze kwao mbinu wanazozitumia kwenye umachinga na kufanikiwa haraka alafu tuwaige na aikwezekana tuwaoe mabinti wa kichina ili tupate hybridge itakayobadilisha hiki kizazi chetu.

Tukikomaa na kuendelea kuamini kwamba twatenda sawa tunakosea kwani tutajikuta tupo kwenye kisiwa na kutofahamu mbinu mbadala za kuleta maendeleo
 
By the way Watanzania si wapo China wanafanya biashara kawa wao, tubadilishe elimu yetu ya kukariri tuzione fursa kupita wao tuone kama watakaa hapa.Kuwafukuza wachina ni ubaguzi kama anaofanya yule mwanasiasa anayetaka Wachaga wasichaguliwe Arusha.Wachina wabaki watufundishe kuwa nchi hii ni tajiri tatizo ni umaskini wetu wa mawazo
 
Duh humu naona TIC na Fair competition act duh labda mi nigusie sheria ya uhamiaji...wakati hao wachina wakitafuta vibali (visa) vya kuja nchini naamini walisema wanakuja kufanya nini lakini sidhani kwamba walisema wanakuja kutembeza simu, kwa hiyo kama sheria ya uwekezaji ikishindwa kuwabana basi kwenye sheria ya uhamiaji hawaruki.
 
Kumekuwa na matamko mbali mbali yakikemea raia kutoka china wasijihusishe na kufanya biashara ndogo ndogo, hivi kufanya biashara ndogongodo ukiwa raia wa nche ni kosa kwa mujibu wa sheria gani. Ninavyofahamu mimi Fair competition Act ya 2003 inazuia uingizaji wa bidhaa zisizofikia kiwango lakini sheria hii haielezi kwamba kuwa raia wa nje haruhusiwi kufanya biashara nchini. Kuna kisingizio kingine kwamba wachina wanaingia nchini kwa kisingizio cha 'investors' only to find them hawking lakini kwa mujibu wa TIC ACT investors ni wale wenye mtaji kuanzia dola 100,000. Je wachina kuja nchini kufanya biashara wamevunja sheria gani?

Wachina hawaji na dola 100,000 most of them,na taarifa ingine ni kwamba wachina hawa kuanzia uko kwao sio wafanyabiashara,hawa unaowaona hapa hawajui hata kiingereza inamaana hawajahi kuwa na mipango ya kufanya international business achilia mbali kwamba hata mitaji yao wanapewa na serikali yao-interest free.waende.
 
lakini hawajavunja sheria yeyote na kingine kwanini tusianze kuwa fundisha vijana wetu lugha ya kichina ili wawewanaongea nao kiurahisi..
 
Wachina hawaji na dola 100,000 most of them,na taarifa ingine ni kwamba wachina hawa kuanzia uko kwao sio wafanyabiashara,hawa unaowaona hapa hawajui hata kiingereza inamaana hawajahi kuwa na mipango ya kufanya international business achilia mbali kwamba hata mitaji yao wanapewa na serikali yao-interest free.waende.

Ule ukweli ni Kwamba wachina wanaokuja kisheria ni wale wenye makampuni ya ujenzi lakini sio vibarua wao na wa kkoo wote haramu
 
Kumekuwa na matamko mbali mbali yakikemea raia kutoka china wasijihusishe na kufanya biashara ndogo ndogo, hivi kufanya biashara ndogongodo ukiwa raia wa nche ni kosa kwa mujibu wa sheria gani. Ninavyofahamu mimi Fair competition Act ya 2003 inazuia uingizaji wa bidhaa zisizofikia kiwango lakini sheria hii haielezi kwamba kuwa raia wa nje haruhusiwi kufanya biashara nchini. Kuna kisingizio kingine kwamba wachina wanaingia nchini kwa kisingizio cha 'investors' only to find them hawking lakini kwa mujibu wa TIC ACT investors ni wale wenye mtaji kuanzia dola 100,000. Je wachina kuja nchini kufanya biashara wamevunja sheria gani?
Kufanya biashara per se sidhani kama ni kosa na ndio maana bado wapo wanaendelea.
Lakini namna wanavyoifanya hiyo biashara ndilo linaweza kuwa tatizo

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Wachina hawaji na dola 100,000 most of them,na taarifa ingine ni kwamba wachina hawa kuanzia uko kwao sio wafanyabiashara,hawa unaowaona hapa hawajui hata kiingereza inamaana hawajahi kuwa na mipango ya kufanya international business achilia mbali kwamba hata mitaji yao wanapewa na serikali yao-interest free.waende.
kuna jamaa aliwahi kuniambia kuna baadhi yao huletwa huku kutumikia vifungo vya nje.
 
Ndio maana Ujasiriamali,u'should find the opputunity,competition ya kutafuta rizk china ni ngumu sana,so wanaangalia maeneo ambayo ushindani ni mdogo ili wakatafute huko,ndio maana machinga wa Kichina wanapatikana karibu Nchi nyingi za Africa,so chamsingi ni tujifunze tech yao ili nasi tujenge taifa letu.
 
Back
Top Bottom