Wachezaji watatu mahiri kuwahi kucheza Simba SC

Steven Nemes
Mwakalebela
Kasongo Athumani
Kenneth Mkapa
Salvator Edward
Edibily Lunyamila
Thomas Kipese
Joseph Lazaro - Tungaraza
Mohammed Hussein "Mmachinga"
 
Kuelekea derby ya Jumamosi ya Yanga Vs Simba, tuwataje wachezaji watatu mahiri na bora kuwahi kuvaa jezi nyekundu na nyeupe za Simba Sc.

  1. Mzee Haidery Abeid....hii midfielder sijawahi kuona Tanzania
  2. Fundi Hussein Aman Marsha...midfielder asiye na mfano kuwahi kutokea nchini Tanzania
  3. Marehemu Hamis Tobius Gaga ' Gagarino '...midfielder aliyekufa na ujuzi wake ambao hauelezeki
 
Mimi nafikiri haya maswali ya namna hii yangekuwa labda yanatenga nyakati ambazo wamecheza . Maana tutajikuta kila mtu anamsemea mcheza wa kizazi chake yaani ambaye amemshudia . Vinginevyo tutakuwa hatuwatendei haki baadhi ya wachezaji ambao hatukubahatika kuwaona . Kila kizazi au enzi inakuwa na wachezaji bora kwa kila timu . Sasa swali la mtoa mada ili lijibike vyema na kuwatendea wachezaji wote haki ni lazima uanzie nyakati ambazo Simba ilianzishwa mnamo 1936 na wote tulioko humu hatukuwa tumefikirika kuwepo .
 
Back
Top Bottom