Jacobus
JF-Expert Member
- Mar 29, 2011
- 4,700
- 1,721
Wakuu, nimekuwa najiuliza TFF ni shirikisho au klabu kama Mtibwa, maana kama TFF ni shirikisho basi tungepewa majina ya wachezaji wa timu za Taifa na vilabu wanavovichezea lakini ni wachezaji wa timu ya wakubwa tu ndo wanatoka katika vilabu tena wengi ni tokea vilabu vitatu tu vya Dar. Wachezaji vijana (wa umri wowote) na wasichana hawa ni kutokana na bonanza tu. Uongozi wa TFF haujajibadilisha na kujiona ni wa taifa lote la Tanzania hivo wanatakiwa kuhakikisha vilabu vyote hasa vya ligi kuu vinakuwa na wachezaji hao wapende wasipende. Kwa mtindo huu basi TFF nayo ishiriki katika ligi maana ni kama klabu. Msikie rais wake alivowaahidi vijana wa Serengeti kana kwamba ni timu yake! Badilikeni, wenzetu hawako hivo. Kuiga vya England tunashindwa basi tujaribu vya Iceland basi.