Wachezaji wa mpira bongo tunaridhika mapema

pogosoXmayhem

New Member
Mar 17, 2017
0
1
Mimi ni kijana wa kitanzania ambae ni muumini mkubwa na muelewa wa mchezo wa mpira wa miguu yaani soka, naupenda mchezo huu pia naweza kuucheza ila co kwa level za kimashindano, napenda kuchukua fursa hii pendwa kuyaelezea yanayonigusa kwenye tasnia hii ya mpira wa miguu, kitu kinachopelekea kudolola kwa timu yetu ya taifa,

Wachezaji wengi wa kitanzania kujituma kwao target kubwa ni kucheza simba na yanga tu ili kupata kujulikana na kuonekana kwenye vyombo vya habari kama magazetini na mitandaoni kila mwisho wa wiki kito ambacho ni tofauti na wana mashariki wenzetu kama Kenya na Uganda, kidogo wao wanaonyesha wanaghadhabu na uchu wa mafanikio pindi pale inapotokea fursa ya kwenda kuonesha walichojaaliwa kwenye mpira nje ya nchi na ndomana mpaka leo tukikutana na mataifa hayo unaona kuna utofauti flani,

Sisi tunapenda kutumia wachezaji wa CAN kwenye friendly match kitu ambacho kinapelekea kutowaamini na kutogundua wachezaji wetu wazawa uwezo wao kwenye mechi hizo, mimi ctaki kuamini kama nchi kama yetu yenye watu wasiopungua milioni 50 tukashindwa kuwa na wachezaji ata 10 kwenye ligi ya SPL ya Afrika ya kusini ili kuweza kuleta ugumu na utofauti kati yao na wachezaji wazawa, leo Samatta,

Ulimwengu na juzi Farid ndo wanaoiwakilisha Tanzania ng'ambo kitu kinacholeta ugumu sana kwa watu watatu tu kuisaidia nchi tunapokutana na nchi kama ivory coast yenye zaidi ya wachezaji 40 ambao wanacheza ligi kubwa na za thamani huko ulaya na kuwepo kwa kikosi chenye mastaa lukuki ndani yake,

Sidhani kama tunaweza kupata matokeo chanya na kutegemea na mifumo ya ligi yetu ya nyumbani inavyoendeshwa cdhani na ctalajii siku Tanzania tukafanikiwa kwenye michuano mikubwa kama AFCON na World Cup, muda ni huu kwa wachezaji wengi vijana ambao wapo kwenye ubora wao kipindi hiki kutafuta matunda kwenye vilabu vikubwa hapa Afrika au nje ya Afrika ili kuleta utofauti kati ya mchezaji wa CHAN na CAN,

Naamini kwenye upande wa CHAN tupo vizuri kidogo ila inatubidi tuoneshe hasira kwamba hatujaridhika na hapa tulipo.

[HASHTAG]#simon[/HASHTAG] msuva [HASHTAG]#jonas[/HASHTAG] mkude [HASHTAG]#saidi[/HASHTAG] ndemla [HASHTAG]#himid[/HASHTAG] mao # ibrahim ajib [HASHTAG]#mohamed[/HASHTAG] hussein [HASHTAG]#sure[/HASHTAG] boi [HASHTAG]#shomari[/HASHTAG] kapombe [HASHTAG]#mbaraka[/HASHTAG] yusufu [HASHTAG]#aishi[/HASHTAG] manura [HASHTAG]#deogratius[/HASHTAG] munish.

wapo wengi sana ila hawa muda wao umefika ningependa kuona mpaka mwakani hawa niliowaorodhesha hapa kwenda kukipiga kwenye timu kubwa nje ya nchi.
 
Back
Top Bottom