Wachezaji wa Afrika kugoma kujiunga na timu zao za Taifa

bryan2

JF-Expert Member
Jun 8, 2016
3,321
4,671
Hii ni tofauti kidogo na wenzetu wazungu wakati wao wakitamani kuitwa timu zao za taifa kwetu Gondwanaland(Afrika) ni tofauti

Zikibaki siku kadhaa Kombe la Mataifa Huru la Afrika kuanza kule Gabon baadhi ya Wachezaji wa Timu za Taifa wamegoma kujiunga na timu Zao za Taifa kwa Sababu ambazo hazina mashiko.

Je kugoma huku ni kukosa Uzalendo kwa Wachezaji wa Kiafrika juu ya Nchi zao au kuna lingine la Ziada?

MFANO Zaidi ya Wachezaji watano wa Cameroon(Indomitable lion),Matip Mcameroon anayekipiga Liverpool,NYOM Mcameroon anayekipiga Westbromwich...etc
 
Hii ni tofauti kidogo na wenzetu wazungu wakati wao wakitamani kuitwa timu zao za taifa kwetu Gondwanaland(Afrika) ni tofauti

Zikibaki siku kadhaa Kombe la Mataifa Huru la Afrika kuanza kule Gabon baadhi ya Wachezaji wa Timu za Taifa wamegoma kujiunga na timu Zao za Taifa kwa Sababu ambazo hazina mashiko.

Je kugoma huku ni kukosa Uzalendo kwa Wachezaji wa Kiafrika juu ya Nchi zao au kuna lingine la Ziada?
Nchi za ulaya hata wanapokupa uraia wanakuambia wanaelewa kuwa "your birth country" inaweza kukuhitaji katika timu ya mpira au kwenda kupigana vita, hawawezi kukuzuia ukiamua kufanya hivyo.
 
Mkuu ipe nyama kidogo hii post yako. Wachezaji gani waliogoma?Ungetupa majina na sababu walizotoa ili tuchangie kwa ufanisi na uhakika zaidi.
Wachezaji wa nchi gani wamegoma?..mgomo nini 'posho' kama kawaida yao?
 
Hii ni tofauti kidogo na wenzetu wazungu wakati wao wakitamani kuitwa timu zao za taifa kwetu Gondwanaland(Afrika) ni tofauti

Zikibaki siku kadhaa Kombe la Mataifa Huru la Afrika kuanza kule Gabon baadhi ya Wachezaji wa Timu za Taifa wamegoma kujiunga na timu Zao za Taifa kwa Sababu ambazo hazina mashiko.

Je kugoma huku ni kukosa Uzalendo kwa Wachezaji wa Kiafrika juu ya Nchi zao au kuna lingine la Ziada?
Wanahofia kupoteza namba ktk vilabu vyao CAF walishauriwa michuano ya mataifa ya afrika waihamishie mwezi june wamegoma sasa jamaa wameona ni bora kulinda ugali wao
 
wanaogopa kupoteza namba kwenye vilabu vyao, lakini hebu orodhesha waliogoma
 
Wengi ni wachezaji wa Cameron akiongozwa na beki wa Liverpool, Joel Matip... pande zote mbili ni wapumbavu, wachezaji hata uongozi wa timu za taifa za afrika... nchi zingine watu wanalilia kuitwa kikosi cha taifa ila hali ni tofauti kabisa kwa wachezaji wa bara la giza.. wachezaji hawawatendei haki kabisa raia wa nchi husika.. na uongozi inabidi waangalie dosari yao ni nini hadi wachezaji wanagoma kutumikia taifa lao.
 
Wachezaji wanagomaje? Nijuavyo akiitwa timu ya taifa hawez kugoma maana atafungiwa kwa sheria za FIFA. Matip hakua na uhusiano mzuri na kocha wake ndo maana hajaitwa. Ninachoweza kukubaliana na mtoa post ni kwamba uzalendo umepungua kwa wachezaji wa Africa, hawapambani uwanjani Kama wanavyopambana klabuni.
 
Nahisi kuna harufu ya ufisadi kwenye posho za wachezaji wanazotakiwa kupewa wanapoenda kwenye team ya taifa. Hili tatizo limekua sugu sana kwa Cameroon, ile ni haki yao. Ni system mbovu sana kuwa na ufisadi au kuchelewesha posho za wachezaji maana si kweli kwamba zinachelewa kuifikia mamlaka husika. Africa tuna matatizo mengi sana.
 
Issue ni muda unaofanyika mashindano ligi za ulaya zinaendelea na kama upo first eleven unaweza kukosa namba kama ni mchezaji wa kawaida,watu kama Okocha,Kanu,Drogba,Toure,Etoo walikua wakirudi wanazikuta nafasi zao.John Obi Mikel alienda kucheza Olympic mpaka leo anachoma mahind Darajani ingawa mwenyewe anadai hajutii kwenda Olympics
 
Zamani haya mashindano yalikuwa na msisimko sana,hata hapa nyumbani pia TV station nyingi zilikuwa zinaonyesha na kuzungumzia sana,Mpaka leo hakuna TV station inayotangaza kuwa itaonyesha LIVE,
 
Back
Top Bottom