Mario Kejob
JF-Expert Member
- Apr 14, 2020
- 441
- 536
Kwa sisi washabiki wa zama hizo tuliowaona Sunday Manara na King Kibaden wakicheza, haikuwa jambo rahisi kwa mchezaji kuhama Yanga kwenda Simba au Simba kwenda Yanga.
Wachezaji walijiunga na vilabu hivi kwa mapenzi yao na vilabu hivyo na hivyo kujitoa kwa moyo wote wakati wakichezea vilabu hivyo.
Mambo yaliyozuka siku hizi kwa mfano kumuona Ajibu Akichezea Simba msimu huu na msimu unaofuata akichezea Yanga yanapunguza ushabiki na hata thamani na upenzi wa mchezaji. Enzi hizo huu ulikuwa ni usaliti mkubwa.
Tumeyaona haya pia kwa Niyonzima na nenda rudi zake na labda hivi karibuni yatajirudia tena kwa Shishimbi na Morrison.
Mimi kama mshabiki wa Simba silifurahii swala hili kabisa na kama Yanga imewaacha wangeenda tu vilabu vingine kama Azam ambayo ingekuwa inawahitaji.
Na wala sioni haja yoyote kama Simba inawahitaji wachezaji hao kwa sasa kwani team inaonekana iko vizuri tu.
Hivyo, nawaomba viongozi wa Simba kama walikuwa na mpango huo waufutilie mbali kabisa kwani hauna tija yoyote kwenye club.