Wachambuzi wa michezo kwenye Tv zetu

GREGO

JF-Expert Member
Apr 3, 2014
4,279
2,913
Habari wanaJF
Najiuliza swali kuhusu hawa wachambuzi wa michezo kwenye TV zetu kama Azam TV

Je, ni kweli kwamba mchambuzi mmoja anaweza kuwa na uelewa wa kuchambua michezo yote nikimaanisha Football, Basketball, Volleyball, kuogelea, kickboxing, kukimbia, mieleka, cricket, tenis, Vinyoya, n.k

Nawasilisha
 
Sio wachambuzi
ni sports journalists ....
Ahsante mkuu

Ila nashangaa hawa jamaa wa Azamu TV wanajiita wachambuzi ila wanachambua michezo yote nivtofauti na Dr. Leacky alivyokua enzi zake alibase zaidi kwenye football
 
Dr. Leacky alikuwa anaenda kushudia game za liver live, aliongea anachojua, hawa wavimba macho waliobaki ni hovyo
 
Shafii dauda anajifanya jembeee wakat kazi kudesa tuu goal.com na kujafanyaaa mjuaji....
 
tatizo sio wao
tatizo liko vyuo vya uandishi wa habari
hakuna specialization

ndo maana ezekiel Kamwaga yupo kwenye politics'
sports hadi movies na music...
Hapa nimekupata na wengine hawaendi hata vyuoni mtu anaongea sio kuchambua nanukuu "utasikia sikushangaa maana nilitegemea kitu kama kile kutokea" yaani hadi tabu kuwaelewa
 
Shafii dauda anajifanya jembeee wakat kazi kudesa tuu goal.com na kujafanyaaa mjuaji....
aaaaaahahahhaha na sofascore flash score na livescores.com.

ila mkuu sasa ulitaka wanayochambua wayatoe wapi ilihali hakuna bongo app inayofanya vizuri kwenye michezo hususani swala la uchambuzi?
 
Ukimlaumu shaffih eti anachambua kwa kupata taarifa mitandaoni lazima utakuwa una chuki binafsi au matatizo yako mwenyewe...


Unategemea zaarifa apate wapi sasa... awe anajitungia au... maana kuna sehemu kama mchambuzi anatoa mawazo yake ila sehemu kubwa ya uchambuzi lazima itokane na data utakazopata
 
Back
Top Bottom