MM pia sio mchaga, lakini ni vizuri uwe na heshima kuto-generalize story za kijiweni na marafiki zako halafu unaandika utumbo. Kauli yako ya mwanzo ni upuuzi, lakini kwa vile hapo kwenye red umeuliza ili uelimishwe ndio kisa cha mimi kuchangia. Ni kweli viazi hivyo vipo, vinaitwa viazi vikuu. Nimeambatanisha picha uki-zoom utaona hivyo viazi vina umbo la mviringo ingawa sio smooth. Picha hii nimepiga mwenyewe Kirua Vunjo kule mlimani karibu na Marua.
Yuko sahihi ni kiazi hata wazungu wanaita 'air potato'. Ni sahihi vinaliwa na vina radha inakaribiana sana na viazi wa mviringo Angalia hapo utapata maana yake halisi. Muwe na siku njema .
Machalari tena" nazani bado huvijui.
Nduu ni tofauti na maduma ( soo) zenyewe ni white nduu zina rangi ya njano upishi wake huwa hazimenywi huchemshwa tuu.
Dah! Nakumbukaga miaka iyo kama amna kitafunwa asubuhi bibi alikuwa anavichemsha tunanywea chai sasa vilivyo vichungu kama clorokwini lkn nahisi ni dawa Kwa miili yetu
Dah elimu? Nakimbuka mbali pia tulikuwa tukienda kukata Majani mtoni unakutana na straberrry unajichumia unajilia uku dar pale kisutu kikontainer kidogo elf tano sijui nirudi kijijini