Wabunge wetu na kisingizio cha "maslahi ya taifa" | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wabunge wetu na kisingizio cha "maslahi ya taifa"

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Ndusty, Feb 21, 2012.

 1. N

  Ndusty JF-Expert Member

  #1
  Feb 21, 2012
  Joined: Apr 27, 2009
  Messages: 363
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 45
  Wakuu salaam.Nimshuru kabla yoyote ambaye atapata muda wa kupitia hichi ninacho panga kukiwakilisha kwenu mkiwa kama watanzania wenzangu nikiamini kwamba tuna haki ( kila mtu)na majukumu ya kuchangia masuala yanayohusu nchi yetu.kwamba kila mtanzania mzalendo lazima awe responsible na nchi yetu.kwamba matatizo ya serekali yanatuaffect wote na sisi wananchi ndio wenye mamlaka ya kuleta maendeleo na mabadiliko ya nchi yetu.Tujikumbushe kwamba serekali ni mali ya wananchi wote na wale viongozi ambao wanatuongoza ni waajiriwa wetu kwasababu sisi ndio tuliowaweka kwenye hizo nafasi za uongozi. kwahiyo wananchi tukiwa kama waajiri tuna mamlaka ya kuwafukuza kazi pale wanapokuwa wanakwenda kinyume na malengo,maagizo au masharti yetu.kwenye makampuni na taasisi nyingine waajiri huwa wanafukuza wafanyakazi pale wanapokuwa useless.
  Sasa wakuu naomba nirudi kwenye point yangu muhimu.kwenye hili suala la hawa viongozi(waajiriwa) wetu naomba niongelee kuhusu hawa Wabunge wetu na zaidi wabunge ambao ni wakuchaguliwa na sio wabunge maalumu au wakuteuliwa.naongelea hawa wabunge wakuchaguliwa zaidi kwasababu ninaamini kwamba wao zaidi ya wengine wote ndio wakulaumiwa kwa matatizo yetu mengi tuliyokuwa nayo.ndio wakulaumiwa kwa umaskini wetu uliokithiri.
  Kwanini nawalaumu zaidi wabunge?Wakuu kama mashirika,makampuni na taasisi nyinginezo kila mahali duniani kuna system ya uongozi kuanzia chini mpaka juu.hizi system ni kurahisisha na kuleta ufanisi kwenye kazi au mambo mnayo husika nayo.ndio maana serekali yetu ina Raisi,waziri mkuu,mawaziri,wabunge mapak viongozi level ya chini kabisa ili tu kuleta ufanisi kwenye majukumu ya serekali.kwamba kulete ufanisi au maendeleo kwa wananchi ni lazima wale viongozi wote watekeleze majukumu yao ambayo yamewaweka kwenye hivyo vyeo.Mbunge ni mwakilishi wa wananchi.kwamba jukumu au kazi yake ni kuwakilisha matatizo ya wananchi wake wa sehemu alikotokea.mbunge anatakiwa ahakikishe kwamba anasimamia,kuwasilisha na kutatua matatizo ya wale anaowawakilisha.Hatuwezi tukamtupia lawama zote Raisi kwa kushindwa kutuletea maisha bora kwani tutakuwa tunamwonea bure tu.kama kila kiongozi angetekeleza majukumu yake ipasavyo huu umaskini usingekuwepo.kama kila kiongozi anamwachia raisi afanye kila kitu hatuwezi kufika popote.
  Sasa hawa wabunge wetu wamekuwa wakishaingia bungeni wanasahau au wanaacha kufanya kazi tulizo watuma na badala yake wanajipangia majukumu yao wenyewe kulingana na wao wenyewe wanavyopenda.mfano kuna wabunge wamekuwa wakilipwa na watu ili kupitisha bajeti au kukubali kusign mikataba ambayo haina manufaa kwa wananchi.wanangangania kutetea hoja kwa maslahi yao binafsi kwa kutumia kigezo cha maslahi ya taifa.wanakuwa wako busy kunyooshea na kulaumu wenzao huku wakijidai ni kwa maslahi ya taifa.suala la dowans na richmond na matatizo mengine ambayo yalitokea hayana maana au sababu yakuendelea kuyashabikia kwasababu yameshatokea.lakini wabunge wetu wamekuwa kila leo kujidai kuyaongelea pasipo kutoa solution namna gani wasaidie wananchi kukabiliana na matatizo ya ugumu wa maisha yanayowakumba kila siku.hata kama serekali ingerudishiwa pesa zote zilizowahi kutapeliwa hakutafanya wananchi wawe na maisha bora.
  Mbunge mwenye nia nzuri na anayejali maisha ya wananchi waliomtuma bungeni anatakiwa ashughulikie matatizo ya jimboni kwake zaidi.ajaribu kuboresha hali ya wananchi wake wa jimboni kwake kwanza na sio kujaribu kutaka kutatua matatizo ya nchi nzima as if yeye ndiye raisi.kama kila mbunge angekuwa anajitahidi tu kuwakilisha jimbo lake nadhani nchi yetu kila sehemu kungekuwa na maendeleo.tunapenda kuona wabunge wakishinda kuendeleza majimbo yao na sio kushindana kukusoa viongozi wenzao na Raisi wakati wao hawafanyi chochote.zaidi kwa wabunge wa CCM ambao ndio wenye kuendesha serekali.sio kukosoana kila kukicha pasipo kutoa solution.
  Wakuu sijawahi kuona mbunge hata mmoja ambaye amewahi kutuma post hapa JF kuomba mchango wa kuchangia madawati,au ujenzi wa clinic au kuchangia maendeleo ya aina yoyote huko wanakotoka.wabunge wanawaacha kutatua kero za majimbo yao wanajiweka busy kwenye kujidai kutoa hoja ambazo hazina manufaa yoyote kwa wananchi.wao majukumu ya kuleta maendeleo kwa wananchi wao sio kazi yao ni kazi ya Raisi.matatizo mengi ambayo yako ndani ya uwezo wao hawataki kuyafanya.wananchi hawahitaji bajeti ya serekali kujengewa clinic au shule.wanachohitaji ni kiongozi ambaye anaweza kuwamobilize na kuwashirikisha wao ili walete maendeleo.kuna wananchi wengi wenye uwezo wa kuchangia wengine wasiokuwa na uwezo lakini lazima kuwe na influence ya kufanya watu wenye uwezo kushiriki kuleta maendeleo nchini.wabunge wetu hawafikirii kutatua mamatizo yetu ndio maana wamekaa tu kumlaumu raisi kwa hali iliyopo ila wanaosababisha haya matatizo ni wao.
  Wananchi tumefikia sehemu ya sisi kama waajiri tufikie maamuzi ya kuwafukuza kazi wale wabunge wote ambao hawana manufaa kwetu.Positivity and much blessings!
   
Loading...