Informer
JF-Expert Member
- Jul 29, 2006
- 1,599
- 6,670
WABUNGE wawili wa Chama cha Mapinduzi (CCM), wamebainika kuhusika na vitendo vya ujangili wa kuua tembo, jambo linazorotesha vita dhidi ya ujangili inayofanywa na serikali.
Baada ya kufuatilia kwa karibu matukio ya kesi za ujangili tangu mwaka 2009 hadi mwaka huu, imebainika kuwa baadhi ya wanasiasa wamekuwa wakihusishwa na ujangili, huku vyombo vya dola vikipata shida kukabiliana na vita hiyo kutokana na wanasiasa hao kutumia baadhi ya viongozi ndani ya serikali kufanikisha mbinu za ujangili.
Hata hivyo, taarifa zinaeleza kwamba vyombo vya dola vinaendelea kukusanya ushahidi na kufuatilia nyendo za wanasiasa hao (mawaziri wa awamu iliyopita?) kwa lengo la kuhakikisha kwamba wanachukuliwa hatua. Kwa upande mwingine serikali imeazimia kuvunja kabisa mtandao wa ujangili uliowekwa kwa miaka mingi ukihusisha baadhi ya watendaji wa Idara na taasisi zinazopaswa kupambana na ujangili.
Tukio lililoibua upya uchunguzi dhidi ya wahusika wakuu ni lile la kutunguliwa kwa helikopta iliyokuwa ikisaidia walinzi wa Idara ya wanyamapori katika mbuga ya hifadhi ya Mwiba wilayani Meatu.Tukio hilo ambalo lilisababisha kifo cha rubani wake raia wa Uingereza kwa kupigwa risasi na majangili.
Taarifa zaidi zitashushwa hapa JF muda ukiruhusu
==============
Gari mojawapo la kampuni inayomilikiwa na Mbunge anayehusishwa na Ujangili]