Wabunge wawekewe KPI's

Wabunge wawekewe KPI's

Mkere

New Member
Joined
Apr 28, 2010
Posts
3
Reaction score
0
Mimi si mpenzi sana wa siasa wala si mwanachama wa chama chochote na nilipiga kura nilipokuwa na miaka 18 miaka 20 iliyopita na nilipiga kwa vile nilitaka kujaribisha ila sijaona cha mabadiliko yoyote kwa kweli ndio maana huwa sihangaiki kwenda kupanga foleni.

Katika kipindi hiki cha kutaka mabadiliko kuna wabunge wanaotaka kuingia kuwasilisha majimbo yao na kunawanaotaka kubakia kuendelea kwenda kusinzia bungeni.Mimi binafsi ninaonelea kuwa ni wakati muafaka wa wabunge kufanyakazi kiukweli wawekewe KPI ( Key perfomance indicators) ziwe zinakuwa reviewed kila mwaka na kama hujatimiza malengo kwa asilimia 75% unapigwa chini anachaguliwa mbunge mwingine mwenye ufanisi.
Nasema hivi kwanini? Sioni sababu ya mtu kuchaguliwa wakati kuna basic things ambazo unaweza kujituma kuvifanya aidha kwa kuhamasisha watu wa jimbo lako au kutafuta misaada mbali mbali kwa wafanya biashara wa eneo lako bila kugonjea serikali. Vitu muhimu kama Zahanati, shule, maji na mambo mengine madogo madogo kwa kweli huwa nasikia uchungu sana kwamba tangu nimezaliwa shida ni zile zile hadi leo hii naelekea uzeeni.
Kwa wabunge vijana na wazee wa chama chochote kile wekeni KPI's kwa wawakilishi wenu muwa tathmini baada kipindi maalum, laasivyo mtajaza wauza sura, mafisadi, wasinziaji na wahongaji lazima ifikie wakati mtu uchaguliwe kwa ulichofanya tena kwa kiasi kikubwa ili tunapokuchagua tena tunajua tunachagua nini hapo ndio maendeleo yatapatikana wakati wa kubebana umekwisha

Amani kwenu, mfungo mwema na uchaguzi mwema
 
Good idea,

Tatizo inabidi tuondokane na utamaduni wa "Data Not Available" na tuwe makini sana na jinsi gani hizi data zinapatikana, tusije kupewa data za economic growth ya kwenye makaratasi ambayo haionekani maishani mwa watu kama serikali ya Mkapa.
 
Mimi si mpenzi sana wa siasa wala si mwanachama wa chama chochote na nilipiga kura nilipokuwa na miaka 18 miaka 20 iliyopita na nilipiga kwa vile nilitaka kujaribisha ila sijaona cha mabadiliko yoyote kwa kweli ndio maana huwa sihangaiki kwenda kupanga foleni.

Katika kipindi hiki cha kutaka mabadiliko kuna wabunge wanaotaka kuingia kuwasilisha majimbo yao na kunawanaotaka kubakia kuendelea kwenda kusinzia bungeni.Mimi binafsi ninaonelea kuwa ni wakati muafaka wa wabunge kufanyakazi kiukweli wawekewe KPI ( Key perfomance indicators) ziwe zinakuwa reviewed kila mwaka na kama hujatimiza malengo kwa asilimia 75% unapigwa chini anachaguliwa mbunge mwingine mwenye ufanisi.
Nasema hivi kwanini? Sioni sababu ya mtu kuchaguliwa wakati kuna basic things ambazo unaweza kujituma kuvifanya aidha kwa kuhamasisha watu wa jimbo lako au kutafuta misaada mbali mbali kwa wafanya biashara wa eneo lako bila kugonjea serikali. Vitu muhimu kama Zahanati, shule, maji na mambo mengine madogo madogo kwa kweli huwa nasikia uchungu sana kwamba tangu nimezaliwa shida ni zile zile hadi leo hii naelekea uzeeni.
Kwa wabunge vijana na wazee wa chama chochote kile wekeni KPI's kwa wawakilishi wenu muwa tathmini baada kipindi maalum, laasivyo mtajaza wauza sura, mafisadi, wasinziaji na wahongaji lazima ifikie wakati mtu uchaguliwe kwa ulichofanya tena kwa kiasi kikubwa ili tunapokuchagua tena tunajua tunachagua nini hapo ndio maendeleo yatapatikana wakati wa kubebana umekwisha

Amani kwenu, mfungo mwema na uchaguzi mwema

Mkere... umenena kweli lakini wabongo unawajua? Hebu soma hii habari kutoka magazeti ya IPP:

Utafiti wabaini maajabu ya wabunge machachari

Taasisi ya utafiti ya Tunaweza imeelezea kushangazwa kwake na kuanguka vibaya kwa wabunge wengi machachari wa CCM katika kura za maoni ambao wamekuwa wakitoa michango mingi ya kuichachafya serikali ndani ya Bunge.
Vile vile, imeelezea kushangazwa kwake na ushindi wa kishindo waliopata wabunge ambao hawana kawaida ya kuchangia bungeni wala kuuliza maswali.
Hayo yamo katika ripoti ya uchunguzi wa Taasisi hiyo uliofanywa kati ya mwaka 2005 – 2010 kuhusu utendaji wa wabunge.
Meneja wa taasisi hiyo, Hans Hoogeven, aliliambia NIPASHE kuwa hawakutarajia wabunge wengi wanaotoa michango bungeni kuanguka na wale wasiochangia kitu kupata ushindi mkubwa.
Alisema kati ya wabunge 10 wa CCM ambao walikuwa wanaongoza kwa kuuliza maswali mengi, ni watatu tu wamefanikiwa kupita kwenye kura za maoni.
"Tulitarajia kuwa wananchi wanathamini mchango wa wabunge machachari ambao wanatoa michango mingi ya kuikosoa serikali bungeni, lakini hali imekuwa tofauti kabisa na tunashindwa kuelewa kwa nini imekuwa hivyo…
"Ina maana wananchi wanawapenda wabunge wanaokwenda kule kupumzika tu?" alihoji Hoogeven.
Alisema Mbunge wa Igunga (CCM), Rostam Aziz, ndiye anaongoza kundi la wabunge 10 wa CCM ambao huwa hawaulizi maswali bungeni.
Alisema wameshangazwa na ushindi wa Rostam ambaye takwimu za tangu mwaka 2005, zinaonyesha kuwa hajawahi kuuliza hata swali moja.
Aliwataja wabunge wa CCM walioanguka kwenye kura za maoni ingawa wamekuwa wakichangia kwa wingi bungeni kuwa ni Mgana Msindai (Iramba Mashariki) aliyeuliza maswali 222 kwa kipindi hicho cha miaka mitano.
Wengine na idadi ya maswali waliyouliza na majimbo yao kwenye mabano ni George Lubeleje (Mpwapwa -197), Juma Kilimbah (Iramba Magharibi -196), William Shellukindo (Bumbuli -187), Profesa Benedict Mwalyosi (Ludewa -171), Siraju Kaboyonga (Tabora Mjini -162) na Mohamed Rished Abdalah (Pangani -147).
Alitaja majina ya wabunge wa CCM ambao wanaongoza kwa kutouliza maswali tangu Bunge lianze kazi 2005 na ambao wameshinda kuwa ni Rostam Aziz (Igunga- 0), Mossy Suleiman Mussa (Mfenesini -3), Salum Khamis Salum (Meatu- 4), Juma Suleiman N'hunga (Dole-5), Lolesia Bukwimba (Busanda -5), Hassan Rajabu Khatib (Amani - 6), Omar Sheha Musa (Chumbuni -7), Abdalah Sumry (Mpanda Magharibi -7), William Kusila (Bahi -9) na Mohamed Dewji (Sindiga Mjini -10).
Kwa ujumla, Hoogeveen, alisema aliyekuwa Mbunge wa Karatu (Chadema), Dk. Willibroad Slaa, ndiye anaongoza kwa kuichachafya serikali kwa maswali ya msingi na nyongeza.
Alisema mbunge huyo aliuliza maswali 33 ya msingi tangu mwaka 2005, maswali 268 ya nyongeza na ametoa michango kadhaa bungeni mara 129.
Alisema Dk. Slaa ni miongoni mwa wabunge ambao wamekuwa wakitimiza wajibu wao ipasavyo kuiwajibisha serikali ili isimamie masuala ya maendeleo.
"Bila wabunge machachari kama Dk. Slaa tusingejua kashfa kadhaa kama ufisadi wa Benki Kuu, EPA, Richmond na maovu mengine mengi ambayo yaliibuliwa bungeni…Bunge linatumia gharama kubwa kujiendesha hivyo lazima watu wafanye kazi, kule bungeni si sehemu ya kupumzika," alisema Hoogeveen.
"Maana ya mbunge ni kuchangia kuikosoa serikali inapoonyesha udhaifu katika utendaji, sasa kama mbunge haulizi maswali amekwenda kufanya nini bungeni?" alihoji na kuongeza kuwa wameshangazwa na anguko la wabunge waliochangia kwa wingi na waliokuwa mstari wa mbele kuikosoa serikali.
Alisema matokeo hayo ya uchunguzi yanaacha maswali mengi kuhusu wajibu na kazi za Bunge na chaguo la wana CCM ambao walipiga kura kwenye kura za maoni hivi karibuni.
Alisema ripoti hiyo inaacha swali kuwa ni kwa vipi wabunge wa CCM wanatathiminiwa katika kazi ya kuiwajibisha serikali ndani ya Bunge.
Sasa wewe jiulize vibudu kama Rostam na Dewji ndio wamepeta hawana akili mzuri...
 
Hili ni wazo zuri lakini. Siku zote najiuliza kazi ya mbunge hasa ni nini? Sijui jibu nililonalo kama ni jibu sahihi.

Je Matatizo ya umeme kigoma ni sababu hawakua na wabunge wazuri. Je bara bara za lami na umeme Kilimanjaro vijijini ni KPI kuonyesha wabunge wa moshi ni wamekuwa watendaji wazuri?

Je kuna wabunge wana ujanja wa kulobby miradi iliyotakiwa kwenda sehemu fulani iende jimboni kwao ? Vipimo vya KPI za wabunge mawaziri zitakuwa sawa na wale wasio mawaziri?Kuna maswali mengi

Binafsi naona mchango wa wabunge kwenye maendeleo ya wananchi ni mdogo sana. Infact naona bunge la tanzania linatakiw kuwa na wabunge kati ya 100-125.Sababu matatizo tuliyonayo ni yale yale. Ni sehemu chache sana zina area specific problem. Hizi KPI labda tuziweke kwa ma DC na RC

Kuna old guard mmoja wa CCM (kati ya Malecela / Kingune/ Rostam nafikiri, can't be sure), aliulizwa anawezaje kuwa mbunge bila kuuliza maswali mengi bungeni? Mbona hasikiki?

Akajibu na kusema kwamba, kuna backroom dealins na mawaziri zinaweza kuwa muhimu kuliko hata maswali bungeni, na mara nyingi hata wabunge wanaouliza maswali hufanya hivyo kwa show tu, na kwamba mbunge anaweza asisikike bungeni lakini vitu vyake vikaonekana jimboni, na mwingine akasikika sana bungeni, lakini ikawa lip service tu, jimboni hamna kitu.

Ndiyo mambo ya kina Magufuli hayo, kama waziri huwezi kumsikia anaibana serikali, lakini backroom huko anapiga deals na mawaziri wenzake, hata barabara anaipindisha ipitie jimboni kwake. Sasa utasema mtu kama huyu anahitaji kusikika sana bungeni ?

Najua it sounds a tad bit unethical kwamba kuna level fulani ya transparency inakosekana, lakini inaonekana ndivyo politics za bongo zinavyoenda.
 
mawazo mazuri mdau ila nhi yetu kiziwi kila kitu mpaka kwa hisani ya watu wa marekani
 
Ni kweli kama unavyosema ni show wananchi wajisikie kuwa serikali ipo karibu yao lakini hakuna kitu.

Kwa mahesabu ya haraka nilikuwa naona gharama za mshahara wa mbunge na gharama za uchaguzi za wabunge kwenye jimbo sijui ni shilingi ngapi. But let say kila wilaya inapunguza jimbo Moja. Gharama zinazookolewa zinaweza kujenga visima vya majsafi kwa mwaka katika wilaya. kwa miaka mitano visima 60.

Je kuna wilaya yeyote tanzania japo inajenga visima 10 vya maji kwa. Je kuna mbunge yuko tayari kusimama bungeni kuomba idadi ya majimbo ipunguzwe ai jimbo lake lifutwe na kuomba pesa zitazookolewa ziingie kwenye miradi ya kuwasaidia wanachi?

Tanzania sidhani kama tuna area specific problem kiasi kuhitaji kuwa na wabunge wengi kama tulionao. matatizo yetu ni ya msingi, maji,elimu, afya miundombinu, kilimo.

Wenzetu wanahitaji wabunge wengi sababu matatizo haya walishayamaliza. Kwao kila eneo lina matatizo tofauti. sisi hatujafika uko.

Napenda nisikie NEC inaachana na hizi siasa za kuongeza majimbo.
 
Kuna old guard mmoja wa CCM (kati ya Malecela / Kingune/ Rostam nafikiri, can't be sure), aliulizwa anawezaje kuwa mbunge bila kuuliza maswali mengi bungeni? Mbona hasikiki?

Akajibu na kusema kwamba, kuna backroom dealins na mawaziri zinaweza kuwa muhimu kuliko hata maswali bungeni, na mara nyingi hata wabunge wanaouliza maswali hufanya hivyo kwa show tu, na kwamba mbunge anaweza asisikike bungeni lakini vitu vyake vikaonekana jimboni, na mwingine akasikika sana bungeni, lakini ikawa lip service tu, jimboni hamna kitu.

Ndiyo mambo ya kina Magufuli hayo, kama waziri huwezi kumsikia anaibana serikali, lakini backroom huko anapiga deals na mawaziri wenzake, hata barabara anaipindisha ipitie jimboni kwake. Sasa utasema mtu kama huyu anahitaji kusikika sana bungeni ?

Najua it sounds a tad bit unethical kwamba kuna level fulani ya transparency inakosekana, lakini inaonekana ndivyo politics za bongo zinavyoenda.

Hawa ni wabunge type ya akina Rostam, Mkono, Dewji na Mramba. Wanaiba bilions wanajenga kashule ka million 10.....
 
Kumbuka waswahili husema debe tupu haliachi kutika na simba mwenda kimya ndio mla nyama.Kunyamaza kwa mbunge si kwamba hana kitu.There are a thousand and one ways of doing a thing.
 
Back
Top Bottom